2013-01-23 07:27:37

Juma la kuombea Umoja wa Kanisa Siku ya Sita: kutembea kuvuka vikwazo!


Katika siku hii ya sita wazo letu kuu ni kutembea kuvuka vikwazo. Kwenda kwa unyenyekevu na Mungu maana kutembea kuvivuka vikwazo vinavyowagawanya na kuwaharibifu watoto wa Mungu. Waamini wanaokaa katikati ya madhehebu mengi wanafahamu mgawanyiko na maneno yaliyopo kati yao. RealAudioMP3
Migawanyiko hii ya kanisa inasaliti mwono wa Kibiblia wa umoja ambao tumekusanyika wiki hili kuomba. Mtakatifu Paulo aliishi na Jumuia zilizogawanyika za wayahudi na wapagani au watu wa mataifa katika kanisa la mwanzo. Kwa kikwazo hiki na kwa kila kinachofuata, Mtakatifu Paulo anamtangaza Kristo kuwa amani yetu.
Kwa maisha yake amezifanya jamii hizi mbili zilizogawanyika kuwa jamii moja na kuuvunjilia mbali ukuta uliozitenganisha. Mahali pengine Paulo anaandika; kama vile mlivyobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristu. Hakuna tena myahudi wala myunani, mtumwa au mtu huru, mwanamke au mwanaume; kwa kuwa ninyi nyote ni wamoja katika Kristo.(Wagalatia 3.27-28).
Katika Kristo, mipaka yote mikuu ya ulimwengu wa kale na ile iliyofuata imeondolewa kwa sababu kwa njia ya Msalaba Yesu mwenyewe ameumba ubinadamu mpya. Katika ulimwengu ambao vikwazo vya kidini ni vingi na ni vigumu kuvivuka vyote, Wakristo ambao ni wachache sana katikati ya dini nyingi, unatukumbusha umuhimu wa mazungumzo na ushirikiano kati ya dini mbalimbali.
Injili ya Mathayo inaelezea safari ngumu kwa Yesu na wanafunzi wake kwa kuvuka vikwazo vya dini, utamaduni na jinsia wakati amekutana na mwanamke Mkanaani anayemuomba amsaidie kumtibu binti yake. Silika ya wanafunzi ni kumfukuza mwanamke. Yesu anasita.
Lakini silika ya kumfukuza na kusita kunatambu kwa na imani ya yule mwanamke na hitaji lake kubwa. Kutoka hapa Yesu na wanafunzi wake walikuwa na uwezo wa kuvuka vikwazo na mipaka iliyowekwa na vizazi vilivyopita. Mifano hiyo ipo tayari katika Biblia ya kiyahudi. Katika Kitabu cha Ruthu, mwanamke wa kabila la wamoabu, wa utamaduni na dini tofauti, kinahitimisha orodha ya ukoo wake na Boazi ambaye alikuwa Mwisraeli. Mtoto wao Obedi alikuwa ndiye baba wa Yese, aliyemzaa Daudi.
Ukoo wa Mfalme shujaa wa Israeli ya kale unaonyesha ukweli kwamba mapenzi ya Mungu yanaweza kutimizwa watu wakivuka vikwazo vya dini na utamaduni. kutembea na Mungu hivi leo kunatuhitaji tuvuke vikwazo na tofauti zilizopo kati yetu sisi wakristo kwanza na kati yetu Wakristo na watu wa imani zingine. Kutembea kuelekea umoja wa wakristo kunahitaji kutembea kwa unyenyekevu na Mungu kutambuka vikwazo ambavyo vinatutenga na watu wengine.
SALA
Ee Baba Mungu, utusamehe kwa vikwazo vya uchu, chuki, na dharau tunayojenga daima na ambayo inatutenganisha ndani ya nafsi zetu na ndani ya Makanisa, kati ya watu wa imani zingine, na kutoka kwa wale tunaowafikiria kuwa ni wa muhimu kidogo kuliko sisi.
Roho wako Mtakatifu atupe ujasiri wa kuvuka mipaka hii, na kuziondoa kuta ambazo zinatutenganisha mmoja kwa mwingine. Kisha pamoja na Kristo tunaweza kubeba ujumbe wake wa Upendo na Umoja unaowakubali wote kwa ulimwengu wote. Mungu wa uzima, utuongoze katika njia ya haki na amani. Amina.

MASWALI
Je, ni vikwazo gani vinavyowatenganisha Wakristo katika jamii yako?
Je, ni vikwazo gani vinavyowatenganisha wakristu kutoka na tamaduni na mila zingine za kidini katika jamii yako?
Je, kuna tofauti gani kati ya kutembea kutambuka vikwazo vinavyowatenganisha wakristu wao kwa wao na vinavyowatenganisha wakristu na dini zingine?
Tafakari hii imeandaliwa na Padre Emmanuel Nyaumba.
All the contents on this site are copyrighted ©.