2013-01-22 15:11:05

Vatican yalalamikia mahakama ya Ulaya kumnyima haki ya uhuru wa kidini- Mlalamikaji .


Vatican pamoja na kusifu Mahakama ya Ulaya kwa kutambua na kuwa mtetezi mkubwa wa haki msingi za Binadamu, hivi karibuni haikufurahishwa na maamuzi ya mahakama hiyo , yaliyomnyima haki ya kidhamiri Mfanyakazi wa Shirika la ndege wa Shirika la Bristish Airline, aliyezuiwa kuvaa msalaba juu ya sare za kazi. Vatican imeyaita maamuzi yaliyotolewa na Mahakama hiyo ya Ulaya kuwa ni kuenzi ubaguzi wa kidini nchini Uingereza.
Askofu Mkuu Dominique Mamberti, Katibu wa Vatican kwa ajili ya mahusiano na mataifa, ameeleza na kutaja kwa jinsi ilivyo vigumu kwa kesi zinazohusiana na masuala ya uhuru wa dhamiri na dini, kupata haki hasa katika jamii ya Ulaya, ambayo kwa sasa inazidi kumezwa na tofauti za kidini na hali ngumu zinazoendana na ukana Mungu.
Alieleza na kutoa mfano wa mambo mengine ya kidhamiri yenye utata kimaadili, kama vile utoaji mimba na ushoga, na hivyo akasisitiza uhuru wa dhamiri lazima uheshimiwe,"
Askofu Mkuu alitoa maoni hayo akielnga katika maamuzi ya mahakama wa Ulaya ya Januari 15, kuhusu madai ya manne ya ubaguzi wa dini dhidi ya Wakristo Uingereza,ikiwemo kesi ya Nadia Eweida, 60, Mkristo Coptic, aliyezuiwa na mwajiri wake, British Airways, kuvaa msalaba juu ya sare ya kazi ya shirika hilo.
All the contents on this site are copyrighted ©.