2013-01-22 08:23:20

Salam na matashi mema kwa Patriaki Ibrahim Isaac Sidrak


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemwandikia barua ya salam na matashi mema Patriaki Ibrahim Isaac Sidrak, aliyeteuliwa na kuthibitishwa rasmi kuwa Patriaki Mpya wa Kanisa la Kikoptic la Alexandria, Misri. Katika ujumbe wake, Baba Mtakatifu anasema kwamba, kuchaguliwa kwake kuwa Patriaki ni tukio la furaha kwa Kanisa zima. Katika barua hii, anaridhia umoja wa Kikanisa mintarafu mapokeo ya Kanisa Katoliki.

Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kwamba, kwa njia ya Yesu Kristo, aliyeshinda dhambi na mauti kwa njia ya Ufufuko wake na kwa ushirikiano na Mababa wa Sinodi na umoja wa Maaskofu, atakuwa na ujasiri wa kuongoza Kanisa la Kikoptik nchini Misri.

Baba Mtakatifu anamwombea ili aweze kutekeleza utume wake kama Baba na Mkuu wa Kanisa, daima akitangaza Neno la Mungu, ili watu waweze kulimwilisha na kuliadhimisha kwa njia ya Ibada mintarafu Mapokeo na Maadhimisho ya Liturujia ya Kikoptik. Ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, waamini wataweza kupata faraja pamoja na kuonja upendo wa Kibaba kutoka kwa Patriaki mpya.All the contents on this site are copyrighted ©.