2013-01-22 15:02:14

Kardinali Ravasi kuongoza Mafungo ya kiroho ya Papa na Curia


Kardinali Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili a Utamaduni , atakuwa Mhubiri wa mafungo ya Papa ya wiki moja tangu tarehe 17 hadi 23 Februari, kwa ajili ya kuikianza kipindi cha kwaresima kwa mwaka huu 2013. Mahubiri yake yataongozwa na Mada: Sura ya Mungu ni Sura ya Muumini katika Zaburi ” Ars Orandi Ars Credendi”.
Kardinali Ravasi ametaja sababu ya kuchagua aya hiyo ya zaburi akisema, ni kwa kuwa, katika sala, Mungu na Binadamu hukutana na kujadiliana. Na kwake yeye anaiona ni heshima kubwa kuchaguliwa na Papa kuwa mhubiri wake katika kukianza kipindi hiki muhimu cha Kanisa. Na hivyo ni katika mwamko huo wa kiroho, pia kibindamu linamsisimua kuzama katika kina cha tafakari kwa ajili ya kipindi hiki cha Kwaresima. Na pia kwa upande mwingine haya ni majadilaino ya ndani ya watu wanaofanyakazi karibu na Papa.
All the contents on this site are copyrighted ©.