2013-01-22 14:54:41

Habari fupi za uteuzi


Baba Mtakatifu amemteua Padre Dario Edoardo Vigano,mwenye umri wa miaka 51, kuwa Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Runinga cha Vatican. Padre Dario, ni Padre wa Jimbo Kuu la Milan na anachukua nafasi inayoachwa wazi na Mkurugenzi wa sasa Padre Federico Lombardi mwenye umri wa miaka 71, anayestaafu kwa mujibu wa umri.
Aidha Baba Mtakatifu amemteua Mwana Habari Mlei, Dk Angelo Scelzo, kuwa Naibu Mkurugenzi wa Ofisi ya Habari ya Jimbo la Papa. Hadi kuteuliwa kwake, alikuwa Katibu mwandamizi katika Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano Jamii.
Na pia Papa amemteua Mons. Gerardo Antonazzo , Padre wa Jimbo la Ugento – Santa Maria di Leuca, kuwa Askofu wa Jimbo la Sora- Aquino Pontecorvo, Italia. Hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Vika Mkuu w Jimbo hilo.
All the contents on this site are copyrighted ©.