2013-01-21 08:22:55

Umoja wa Wakristo unahitaji: sala, haki na ukarimu!


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, anaendelea kutoa changamoto chanya kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, kwa kuunganisha mapokeo na mambo ya kisasa; kwa kutumia lugha ya maendeleo ya sayansi na teknolojia ya habari pamoja na lugha ya Kilatini, ambayo wengi walidhani kwamba, imekufa na haina tena nafasi katika Karne ya Ishirini na moja.

Hadi sasa akaunti ya Baba Mtakatifu inawafuasi zaidi ya Millioni mbili na nusu, wanaoendelea kuwasiliana kwa lugha ya: Kiingereza, Kiarabu, Kifaransa, Kijerumani, Kireno, Kipolandi na hivi karibuni, “amejimwaga kwenye mtandao kwa kutumia lugha ya Kilatini, kwa kusema kwamba, kwa hakika mtandao wa Twitter kuwa ni mtandao unaotumia maneno machache, lakini ujumbe unafika kwa walengwa.

“Tuus adventus in paginam publicam Summi Pontificis Benedicti XVI breviloquentis optatissimus est” Kwa Lugha ya Kiswahili kwa msaada ya Wazee waliosoma Seminari kuu ya Katigondo, Uganda, tunaweza kusema, “Uwepo wako rasmi Papa Benedikto XVI katika ukurasa wa mtandao wa Twitter ni jambo la kupendeza”.

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, katika Juma hili la kuombea Umoja wa wakristo anabainisha kwamba, Umoja wa Wakristo unahitaji sala, haki na utashi wa kutembea pamoja na Mwenyezi Mungu.

All the contents on this site are copyrighted ©.