2013-01-21 15:13:46

Sala ya Kuombea Umoja wa Wakristu: wito wa kujenga amani duniani – Papa


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, ametoa wito wa kusitishwa kwa ghasia, mizozo na mapigano yenye kudhulumu haki ya watu kuishi kwa amani na utulivu duniani. Ombi hilo alirudia kulitoa mbele ya mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa kanisa kuu la mtaktifu Petro siku ya Jumapili, adhuhuri wakati wa sala ya Malaika wa Bwana.

Papa alikemea ghasia zinazo endelea kusikika pande mbalimbali za dunia ambako umwagaji wa damu ya watu wasiokuwa na hatia unaendelea kusikika licha kusababisha mahangaiko makubwa ya maisha , watu wakikimbia maeneo yao na kwenda kuishi katika hali za dhiki ili mradi wasalimishe maisha yao. Alisali, ili mioyo ya wahusika iguswe na ushupavu wa kuketi katika majadiliano kwa ajili ya maridhiano, na hivyo kusitisha mizozo na ghasia na kudumisha amani.

Papa aliomba amani huku akirejea tafakari za Kanisa katika hoja ya kidharura ya kutafuta umoja kamili wa kuonekana Wakristu , kama Yesu Mwenyewe alivyotamani kwa ajili ya Kanisa lake na kusali -“Baba wale ulionipa, na wawe wamoja kama sisi tulivyo na umoja”.

Jumapili iliyopita , ambayo ilikuwa ni Jumapili ya kwanza ya Kipindi cha Kawaida katika Kalenda ya liturujia ya Kanisa,baada ya kipindi cha majilio na Siku Kuu za Noel, pia ilikuwa ni Siku ya Nne, katika Wiki la Sala kwa ajili ya kuombea Umoja wa Wakristu.
Papa ametoa wito kwa Wakristu wote hasa kwa wiki hili, kushiriki katika sala na maombi ya kiekumene, wakiwa wamejumuika pamoja , kila mmoja akiyatolea maisha yake kwa uaminifu zaidi kwenye kazi zinazo tafuta kufanikisha umoja wa kuonekana wa wafuasi wa Yesu Kristu, Bwana wa Kanisa.
Papa, mara baada ya Malaika wa Bwana, kupitia tovuti ya Tweeter, kwa mara ya kwanza alitoa ujumbe wake katika lugha ya kilatini, kwa ajili ya wiki la kuombea Umoja Kamili wa Wakristu “Unitati christifidelium integre studentes quid iubet Dominus? Orare semper, iustitiam factitare, amare probitatem, humiles Secum ambulare”yaani “ Bwana anatarajia nini katika Umoja wa Wakatistu ? Ni kusali kwa uaminifu , kutenda kwa haki, Matendo ya huruma na kutembea pamoja Nae(. Benedictus PP. XVI ‏@Pontifex_ln).

Wiki ya Kuombea Umoja wa Wakristu, ambalo huadhimishwa kila mwaka tarehe 18 hadi 25 Januari, historia yake ilianzishwa na Paul Irènèe wa Ufaransa katika miaka ya 1890. Wazo lilililotembea hadi mwaka mwaka 1908, ambamo Mchungaji Spencer Jones wa Kanisa la Kianglikan Uingereza na Kadre Lewis Thomas Watton Mwanzilishi wa shirika la Ndugu Wadogo wa Mtaktifu Francis wa kwa pamoja waliweka tarehe 18-25 January kila mwaka kuwa Wiki la Wakristu kuungana nakutolea sala zao kwa ajili ya kuombea Umoja wa Wakristu. Kanisa Katoliki la Roma lilijiunga rasmi katika sala hii, kwa azimio lililopitishwa na Azimio la Baraza la Kiekumeni la Vatican mwaka (1964), matunda ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©.