2013-01-21 15:43:03

Barua kwa Jumuiya ya Mt. Pius X, Mikono ya Papa i wazi kuwapokea


Mahusiano kati ya Jimbo la Papa na Jumuiya ya Mtakatifu Pius X, ni wazi bado kuna matumaini, licha ya utando wa viwingu vya gizagiza uliopo. Ni matumaini yaliyoonyeshwa katika Barua ya hivi karibuni ya Askofu Mkuu Joseph Augustine Di Noia, Makamu wa Rais wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Kanisa la Mungu, Tume inayo wtanya mawasiliana na Jumuiya ya Mtakatifu Pius X, ili wafuasi wa jumuiya hiyo wawe na umoja kamili na Kanisa Katoliki. Jumuiya iliyo undwa na Askofu Mkuu Lefvbre, wa Ufanraza, katika miaka aya 1970, kinyume na taratibu za Jimbo la Papa.
Barua ya Askofu Di Noia, inapatikana katika tovuti ya "Seismograph", kwa Kiingereza na Kifaransa katika kiungo "(ilsismografo.blogspot.it/2013/01/vaticano-texte-integral-de-la-lettre-de.html).

Barua hiyo kimsingi imegawanyika katika sura mbili, majitoleo na udumishaji wa umoja wa Kanisa na nafasi ya Udugu wa kikuhani katika Kanisa , na inakamilika kwa kufanya mapitio katika matatizo ya tangu zamani katika mwanga wa msisitizo wazi unaoonyesha hamu ya Papa Benedikto XVI, kumaliza mvutano uliopo kati ya Kanisa na jumuiya hiyo.
Barua ya Askofu Mkuu Di Noia, inaonyesha kutambua kwamba, licha ya maendeleo yaliyopigwa katika mazungumzo yanayofanywa na Kanisa, "sauti na maudhui" ya taarifa za hivi karibuni, kutoka viongozi wa jumuiya hiyo, zinatia mashaka uwezekano halisi wa upatanisho. Na hivyo kufanya juhudi hizi za majadiliano, kuwa ni ushiriki wa kubadilishana mawazo katika hali za kuheshimiana lakini ndani mwake, hakuna matazamio ya maafikiano kutoka jumuia hiyo.

AskofuMkuu Di Noi anasisitabila kukata tamaa kwamba, , katika mwanga wa Maandiko na Mafundisho ya Kanisa , wajibu wa kudumisha Umoja wa Kanisa wa kweli, ni zawadi ya Roho Mtakatifu ," lakini pia, kunahitajika juhudi za binadamu mwenyewe katika maamuzi yake kuridhia , na matendo yake yaonyeshe ushirikiano huo katika umoja wa Kiroho, na kuchukua hatua za kuonekana dhidi ya roho wa upinzani.

Kwa sababu hii, AskofuMKu Di Noia, ametoa wito wa kutenda kwa fadhila na unyenyekevu, upole na uvumilivu na upendo wa kina, kama msaada katika kutambua wema na nafasi ya wengine, "katika roho ya uchunguzi wazi na nia njema za kiimani .







All the contents on this site are copyrighted ©.