2013-01-19 08:29:49

Wazo kuu katika mafungo ya Kipindi cha Kwaresima 2013: "Uso wa Mungu, Uso wa Mwanadamu katika Sala ya Zaburi"


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, anatarajiwa kuanza mafungo ya Kipindi cha Kwaresima pamoja na wasaidizi wake kuanzia tarehe 17 hadi tarehe 23 Februari 2013 hapa mjini Vatican.

Kwa mwaka huu, mafungo yataongozwa na Kardinali Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa la Utamaduni. Kardinali Ravasi anasema, wazo kuu litakaloongoza mafungo haya ni "uso wa Mungu, uso wa mwanadamu katika Sala ya Zaburi" Kwa lugha ya Kilatini wazo hili linasomeka hivi "Ars orandi, ars credenti".

Kardinali Ravasi anasema, wakati wa mafungo atafafanua kwa kina maneno "kupumua, kufikiri, kupambana na kupenda" mintarafu Sala ya Mzaburi. Ni maneno ya kawaida kabisa yanayotumiwa na binadamu lakini yana maana kubwa sana katika Maandiko Matakatifu, kwani ni mwaliko wa kufanya tafakari ya kina kuhusu Fumbo na mwanga wa Mungu unaoangazia uso wa mwanadamu.







All the contents on this site are copyrighted ©.