2013-01-19 09:14:01

Mamlaka ya Bandari Tanzania na Kampuni ya Reli Tanzania yapata wenyeviti wapya!


Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wapya wa Mamlamka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) . Katika uteuzi huo Rais Kikwete amemteua Prof. Joseph Msambichaka kuwa Mwenyekiti wa TPA na kutengua uteuzi wa Bwana Raphael Mollel, ambaye alikua anashikilia wadhifa huo. Prof. Msambichaka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mbeya.

Rais Vilevile amemteua Bwana Severine M.A Kaombwe, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TRL. Bwana Kaombwe ni Mtaalam wa Usafirishaji (East Africa Corridor Diagnostic Study for Northern and Central Corridors). Kulingana na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peniel Lyimo, uteuzi huu unaanza tarehe 16 Januari, 2013.

All the contents on this site are copyrighted ©.