2013-01-19 08:06:08

Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo siku ya tatu: kutembea kuelekea uhuru


Katika siku hii ya tatu ya kuombea Umoja wa Kanisa, wazo letu kuu ni kutembea kuelekea uhuru. Kutembea kinyenyekevu na Mungu maana yake kuwa daima tayari kupokea uhuru ambao Mungu anaufungua kwa wanadamu wote. RealAudioMP3
Tukiwa na wazo hili tunasherehekea fumbo la kujikomboa kiuhuru yaani kutafuta uhuru wa kweli. Ni fumbo ambalo linatukia hata katika sehemu ambamo manyanyaso, chuki, ubaya na umaskini uliotopea vinaonekana kuwa ni mzigo mkubwa.
Kukataa kabisa kukubali amri na hali za onevu kama zile zilizotolewa na Farao kwa wakunga waliowahudumia watumwa wa kiyahudi inaweza kuonekana kama ni jambo dogo lakini mara nyingi haya ni matendo ambayo yanatukia katika maeneo tunayoishi kila siku.
Hivyo tunasherehekea kupewa uhuru; kwa heshima, kiutu, na kushiriki kikamilifu katika yale yaliyo mema kama yale tunayofanya katika jumuia zetu au tunayojitendea wenyewe. Safari hii ya maisha ya pamoja kuelekea maisha ya kweli ni zawadi ya enjili ya matumaini kwa watu wote. Zawadi hii imejikita katika tofauti zetu katika mfumo wa kutofanana ulimwenguni. Hatua kwa hatua tutaweza kufikia uhuru kutokana na kubaguliwa na kuchukiana.
Ujumbe huu unajieleza vizuri zadi katika simulizi la Yesu na mwanamke msamaria. Mwanamke huyu anatafuta kwanza kujua chanzo cha kubaguliwa na chuki inayomzunguka pia kutafuta njia za kutibu hali hii na mizigo aliyo nayo maishani mwake. Wajibu huu alionao ni mwanzo wa kuongea kwetu na Yesu.
Yesu mwenyewe anaungana naye kuongea naye katika mahitaji yake, ya kiu yake, yanayohitaji msaada, anamfafanulia hali ya kijamii ya kubezwa aliyo nayo ambayo inafanya msaada huu uwe ni shida yake. Pole pole njia ya uhuru inafunguliwa kwa huyu mwanamke kwa vile hali ya maisha yake inatazamwa kwa muelekeo wa Neno la Mungu yaani la Yesu mwenyewe.
Mwisho, mang'amuzi haya yanayarudisha maongezi yao kwenye hatu ambayo inawatenganisha wasamaria na Waisrael yaani mahali pa kuabudia - pale pa kuabudia ni mahali zaidi ya mahali au sehemu inayoonekana. Kuabudu katika roho na kweli ndiko kunahitajika na hapa ndipo tunapojifunza kuwa huru kutokana na yote ambayo yanaturudisha nyuma maishani; kama Wakristo tunaotafuta umoja na kama watu ambao tunapaswa kuzipa changamoto tamaduni zisizokuwa na haki na usawa ndani yake; zinazotufanya watumwa bado na tuliofichika kwa wengine.
Uhuru wetu ndani ya Kristo una sifa ya maisha mapya ndani ya Kristo, maisha ya roho mtakatifu maisha ambayo yanatuwezesha kusimama mbele ya utukufu wa Mungu, kwa nyuso za wazi. Ni katika mwanga huu wa utukufu tunajifunza kujiona sisi kwa sisi kikweli kama tunavyokua katika kuelekea ukomavu au ukamilifu wa umoja wa Kanisa.


SALA:
Ee Mungu unayetupa uhuru asante sana kwa imani iliyojaa ujasiri na matumaini kwa ajili ya wale wanaopambana kuleta heshima na ukamilifu wa maisha. Tunajua kwamba unawainua wale walioanguka na kuwapa uhuru wale waliofungwa. Mwana wako Yesu Kristo anatembea nasi kutuonyesha njia halisi na sahihi ya uhuru. Tunaomba tutambue daima kile ambacho kimetolewa kwetu.
Na tuimarishwe tuweze kuyashinda yaleyanayotufanya watumwa ndani yetu. Mtume Roho wako mtakatifu ili atupe uhuru, ili tukiwa na sauti zilizoungana kwa pamoja tunaweza kutangaza upendo wako kwa ulimwengu. Mungu wa uzima utuongoze katika haki na amani. Amina.
MASWALI:
Je, kuna nyakati katika jumuia zetu za kikristu, ambapo maamuzi mbele na hukumu ya dunia: kuhusiana na rangi, madaraja, jinsia, utaifa, elimu, yanatuzuia kuona barabara mwanga wa utukufu wa Mungu?
Je, ni njia gani ndogo na za kimatendo tunaweza kuzichukua, kama wakristu pamoja, kuleta uhuru wa wana wa Mungu (War 8:21) kwa ajili ya makanisa na jamii kwa mapana?All the contents on this site are copyrighted ©.