Juma la kuombea Umoja wa Wakristo: Siku ya Pili: Kutembea na Mwili wa Kristo unaoteseka
TAFAKARI: Katika siku hii ya pili ya kuombea Umoja wa Wakristo, wazo letu kuu ni kutembea
na mwili wa Kristo unaoteseka. Kuwa wanyenyekevu kwa Mungu maana yake kusikiliza wito unaotuita kutoka katika
sehemu zetu binafsi ya kujistarehesha na kuwasindikiza wengine hasa wanaoteseka.
Maneno ya nabii Ezekiel yanatoa onjeleo ya hali ya maisha ya watu wengi. Mifupa yetu
imekauka na matumaini yetu yametoweka. Tumetengwa. Hata katika maisha yetu nyumbani
mateso yapo yanayotuvunja moyo. Ni kama yale ya Kristo msulubiwa mfuasi wa Kristo
anayashiriki. Watu wa kila nyakati na mataifa wanaoumizwa, Yesu analia kwa ajili
yao: Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha? Wakristo wanaitwa kuishi Njia hii ya
Msalaba. Barua kwa Waebrania inaelezea thamani ya mateso ya Yesu katika wokovu wakati
wa shida nyumbani na ugenini. Yesu anawaita waungane naye. Tunapokutana na wale waliotengwa,
tunamtambua Mungu katika mateso yake. Dira tunayoielekea ni sahihi na wazi. Kuwa
na Kristo maana yake kuwa katika mshikamano hai na wale wanaoteseka. Ndio hawa ambamo
Yesu anashiriki mateso yao. Mwili wa Kristo uliopondeka msalabani kwa ajili yako.
Maisha ya mateso ya Yesu yametanguliwa na karamu ya mwisho. Na hiyo inasherehekewa
kama kama ushindi juu ya mauti katika kila ibada takatifu ya Misa yaani Ekaristi.
Katika adhimisho hili la kikristo Mwili wa Kristo mpondeka unafufuka katika hali ya
mwili wa utukufu. Mwili wake unamegwa ili sisi tuweze kushiriki maisha yake na ndani
yake tunakuwa kitu kimoja. Kama Wakristo tunaotembea kuelekea umoja tunaweza daima
kuona Ekaristi kama sehemu ambapo dhambi ya mgawanyiko ni ya kweli. Tukijua kwamba
hatuwezi sisi kushiriki sakramenti hii pamoja kama tunavyopaswa. Hali hii inatuita
kutafuta nguvu mpya katika mahusiano yetu sisi kwa sisi. Somo la leo linafungua
namna nyingine ya kutafakari. Kutembea na Mwili unaoteseka wa Kristo, yaani na wenye
dhiki, kunafungua umoja wa kiekaristi; kushiriki mkate mmoja na walio na njaa, unavunja
ukuta wa umaskini na ubaguzi, haya pia ni matendo ya kiekaristi. Ambamo wakristo wote
wanaitwa kushiriki na kufanya kazi pamoja. Papa Benedikto wa kumi na sita anaongelea
tafakari yake juu ya Ekaristi kwa ajili ya Kanisa namna hii. Hiyo ni Sakramenti siyo
tu kwa ajili ya kuamini bali kusherehekewa pia (Sakramenti ya upendo). Tukizingatia
maana halisi ya liturjia tunang’amua kwamba hakuna kitu ambacho ni cha kibinadamu
kisichorandana na maisha ya kiekaristi.
SALA Ee Mungu wa huruma, mwana wako
alikufa msalabani ili migawanyiko yetu iweze kuunganishwa. Bado tumemsulibisha mara
nyingi kwa kutengana, kwa mifumo na matendo yanayozuia upendo wako na haki yako kwa
wale wote ambao wamezuiwa kuona zawadi ya uumbaji wako. Umtume roho wako mtakatifu
atuvuvie maisha na kutuponya na utengangano na mmeguko huu ili tuweze kushuhudia pamoja
haki na upendo wa Kristo. Tembea nasi hadi ile siku tutakaposhiriki mkate mmoja na
kikombe kimoja katika meza yako. Mungu wa uzima utuongoze katika njia ya haki na amani.
Amina. MASWALI Kwa taswira ya Manabii ambamo Mungu ametaka haki, kuliko ibada
zisizokuwa na haki tunahitaji kujiuliza maswali: Ni kwa jinsi gani Ekaristi, fumbo
la sadaka ya Kristo na maisha mapya, linalosherehekewa kila mahali tulipo? Je,
tunapaswa kufanya nini kama wakristu kwa pamoja kushuhudia umoja wetu katika Kristo
katika sehemu zinazohitaji msaada wetu wa kuziinua kutoka hali zao duni?