2013-01-19 13:34:18

Askofu Mathieu Madge Lebouakehan ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mouila, Gabon


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amekubali ombi la kung'atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake kutoka kwa Askofu Dominique Bonnet wa Jimbo Katoliki la Mouila, Gabon. Amemteua Askofu Mathieu Madega Lebouakehan kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Mouila kwa kumhamisha kutoka Jimbo Katoliki la Port-Gentil, Gabon.

Askofu Mathieu Lebouakehan ataendelea kuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Port-Gentil, huko Gabon.All the contents on this site are copyrighted ©.