2013-01-18 14:54:33

Patriaki Ibrahim Isaac Sidrak ateuliwa kuliongoza Kanisa Katoliki la kikoptik la Alessandria, Misri


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ameridhia uteuzi wa Patriaki Ibrahim Isaac Sidrak, aliyechaguliwa kisheria na Sinodi hapo tarehe 15 Januari 2013 kuwa Patriaki wa Kanisa Katoliki la Kikoptiki la Alessandria, Misri.

Sinodi ya Maaskofu wa Kikoptiki ilikuwa na kikao chake huko Cairo, Misri kuanzia tarehe 12 hadi tarehe 16 Januari 2013, baada ya Kardinali Antonios Naguib Patriaki wa Alessandria kung'atuka madarakani kutokana na sheria za Kanisa, Baba Mtakatifu pia ameridhia uamuzi huu.

Kabla ya uteuzi huu, Patriaki Ibrahim Isaac Sidrak alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Kikoptiki la Minya, Misri, kufuatia uteuzi uliofanywa kunako tarehe 5 Oktoba 2002 na kuwekwa wakfu tarehe 15 Novemba 2002.All the contents on this site are copyrighted ©.