2013-01-18 14:55:17

Mheshimiwa Padre Andrè Gueye ateuliwa kuwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Thiès, Senegal


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Mheshimiwa Padre Andrè Gueye kutoka Jimbo Katoliki Thiès kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Thiès, nchini Senegal. Hadi uteuzi wake, Askofu mteule alikuwa ni Jaalim wa Falsafa katika Seminari kuu ya St. Jean Marie Vianney iliyoko Jimbo Katoliki la Ziguinchor, Senegal.

Askofu mteule Andrè Gueye alizaliwa tarehe 6 Januari 1967, Jimboni Thiès, Senegal. Baada ya masomo na majiundo yake nchini Senegal na Roma, kunako tarehe 27 Juni 1992 akapewa Daraja Takatifu la Upadre. Tangu wakati huo ametekeleza utume wake wa Kipadre kama Paroko msaidizi, Paroko, na Jaalim. Jimbo Katoliki la Thiès lilikuwa wazi tangu mwaka 2011 kutokana na kifo cha Askofu Sacques Sarr.All the contents on this site are copyrighted ©.