Kanuni msingi katika utoaji wa maoni juu ya mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya Tanzania
Katika utoaji wa maoni ya Katiba Mpya ya Tanzania, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
katika mwongozo wake kuhusu mchakato huu, linawahamasisha waamini na watanzania wote
kuhakikisha kwamba, wanadumisha: umoja na mshikamano wa kitaifa; maelewano na utlivu;
amani na udugu.
Waamini wa
Kanisa Katoliki waendelee kuchangia maoni yao wakizingatia kwa namna ya pekee: utu
na heshima ya kila mtu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu; upendo, mafao ya wengi,
haki msingi za binadamu, ustawi na maendeleo ya wengi nchini Tanzania.
Watanzania
wanahitaji Katiba itakayojibu kero sugu na changamoto ambazo zimekuwa ni kikwazo cha
maendeleo ya wengi; ijielekeze katika kudumisha haki na amani. Katiba mpya iwe ni
ile Katiba inayotekelezeka na kuwajibisha. ibainishe sheria na kanuni za kupambana
na saratani ya rushwa ambayo imejikita katika mihimili ya dola ambayo ni Serikali,
Mahakama na Bunge.