2013-01-17 14:58:25

Askofu mkuu Charles Daniel Balvo ateuliwa kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Kenya na Mwakilishi wa kudumu wa Vatican U.N.E.P, Nairobi


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Askofu mkuu Charles Daniel Balvo kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Kenya na Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilikozoko Nairobi kuhusu mazingira na makazi ya watu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Balvo alikuwa ni Balozi wa Vatican kwenye Visiwa kadhaa kwenye Bahari ya Oceania.

Askofu mkuu Charles Daniel Balvo alizaliwa tarehe 29 Juni 1951 huko Brooklyn, Marekani. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa tarehe 6 Juni 1976. Tarehe Mosi, Aprili 2005.

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, akamteuwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican kwenye Visiwa kadhaa vilivyoko Bahari ya Oceania na hivyo kuwekwa wakfu kuwa Askofu hapo tarehe 29 Juni 2005 na kuanza utume wake wa Kidiplomasia hapo tarehe 25 Machi 2006.All the contents on this site are copyrighted ©.