2013-01-16 14:57:42

Askofu mkuu Joseph Salvador Marino ateuliwa kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Malaysia na Timor Mashariki


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Askofu mkuu Joseph Salvador Marino kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Malaysia na Timor ya Mashariki. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Marino alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Bangaladesh.

Askofu Joseph Salvador Marino alizaliwa tarehe 23 Januari 1953 huko Birmigham, Uingereza. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 25 Agosti 1979. Tarehe 12 Januari 2008, akateuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kuwa Balozi wa Vatican nchini Bangaladesh na kusimikwa kuwa Askofu mkuu tarehe 29 Machi 2008.All the contents on this site are copyrighted ©.