2013-01-10 15:08:52

Majiundo mapya dhidi ya umaskini yajadiliwa kwa kina nchini Gabon


Unyonge, Umaskini na Afrika ni kati ya mada kuu zinazojadiliwa katika mkutano wa kimataifa juu ya majiundo mapya, kama ilivyoandaliwa na Jimbo Katoliki la Port-Gentil , Gabon , kwa lengo la kukuza haki, amani na uchumi kwa jamii ya Afrika.
Askofu Mathieu Mad├Ęga , wa Jimbo Port-Gentil , Jumatano 9 Januari 2013, akiongoza Ibada ya Misa kwa ajili ya kufungua mkutano huo , katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Louis , aliwataka washiriki wa Mkutano huo, kuzichambua kwa makini sababu msingi zinazo dumisha umaskini kwa jamii ya Afrika . Na pia wasiogope kuuzungumzia Umasikini katika tafasiri ya kweli, kwa kuwa Mungu anautambua umaskini wa mtu. Aidha amehimiza bidii ziongezwe katika utoaji wa misaada kwa wahitaji zaidi.
Na Padre Raphael Magloire Mboga, Mratibu wa mkutano huu, aliongeza kwamba, Kanisa linapaswa kuionyesha jamii kwamba, hata katika hali ngumu za kijamii, bado jitihada kuongezwa katika kukabiliana na changamoto za umaskini.
.
Mkutano huu unaokamilika tarehe 16 January 2013, , unahudhuriwa na mamia ya watu mchanganyiko, wakiwa toka Makanisa mbalimbali Wakatoliki, Waprotestant na waislamu. Lengo ni kuzipambanua kwa pamoja mbinu zinazofaa zaidi, kufuta umaskini, duniani na hasa kwa wana wa Afrika.
Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa wa ajili ya Haki na amani, pia atatoa mada katika mkutano huu.
All the contents on this site are copyrighted ©.