2013-01-10 14:51:42

Kuridhia kwa hiari kulitumikia Kanisa, unakuwa wajibu binafsi


Kardinali Leonardo Sandri, Mkuu wa Shirika kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki , akiendelea na ziara yake, Misri, Jumatano alikutana na Viongozi wa kazi za Kitume Misri, nyakati za jioni akiwa mjini Cairo.

Hotuba yake kwa viongozi hao, iliwakumbusha kwamba, ridhia yao kukubali kulitumikia Kanisa, unakuwa ni wajibu binafsi unaodai kulihudumia Kanisa kwa uaminifu, ushirikiano na bidii zaidi, na mshikamano na wachungaji wengine wa Kanisa kwa ajili ya kuihudumia jumuiya Katoliki ya Misri,. Ili kwamba, jumuiya iweze kupata utambuzi na uelewa mpana zaidi juu kupitia maisha ya kisakramenti , Katekesi na matendo ya Huruma, kwa ajili ya wake kwa waume wa Misri.

Kardinali amekiri uwepo wa jangwa la waamini, linalotokana na hali ngumu za kisiasa, zinazo kabili Misri. Na hivyo aliwasihi waliobaki, wawe macho zaidina hali hizo, maana hakuna anayeweza kutabiri kilichofichika katika sura hii ya ukame , katika mitazamo wa kidhamiri na kiroho. Na aliwakumbusha wasiyasahau Maandiko Mataktifu, hasa kwamba, hata siku kabla kutiwa hatiani, Mwana wa Mungu, pia alizama katika ukimwa wa sala kwa Baba yake wa Mbinguni, na ni katika wakati huo makini, wafuasi wake walipomwomba Bwana wao, awafundishe, namna ya kusali.

Kwa namna ya pekee Kardinali Sandri, amewahimiza watunze na kupandikiza imani kwa uthabiti zaidi katika mazinigra yote ya kazi za Kichungaji na kitume , na pengine kujenga ushirikiano wa wazi zaidi kati ya taassii za kikanisa au kama inavyo hamasishwa na shughuli za kichungaji na kitume katika taifa hilo.

Na mwisho aliziweka kazi zao zote katika uaminifu wa mwaka wa Imani , kama ilivyokwisha tangazwa na Baba Mtaktifu Bendikto XV1, hapo Octoba 2012 , na pia kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mtaguso Mku wa Pili wa Vatican .








All the contents on this site are copyrighted ©.