2013-01-09 10:05:52

Rais wa Ghana ameapishwa rasmi kuongoza nchi!


Rais John Mahama wa Ghana aliyeshinda uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo hivi karibuni kwa asilimia 50.7 ya kura zote zilizopigwa, Jumanne, tarehe 8 Januari 2013 ameapishwa rasmi kushika madaraka ya kuwaongoza wananchi wa Ghana kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Matokeo ya uchaguzi yalipingwa vikali na Bwana John Kufour wa Chama cha Upinzani cha N.P.P.

Katika sherehe hizi, Bwana John Kufour alihudhuria pia. Itakumbukwa kwamba, mara baada ya kifo cha Rais John Atta Mills, Bunge la Ghana lilimpitisha Bwana John Mahama kuongoza Ghana katika kipindi cha mpito.All the contents on this site are copyrighted ©.