2013-01-09 15:34:51

Barua ya Shukrani kwa Mama wa Mapadre na Waseminaristi


Kardinali Mauro Piacenza, Mkuu wa Shirika kwa ajili ya Makreli, katika adhimisho la Siku Kuu ya Mwaka mpya , hapo Januari Mosi, ambayo pia ilikuwa ni Siku Kuu ya Mama wa Mungu, alitoa barua ya shukurani maalum, kwa Mama wote wa Mapadre na Waseminaristi wote. Shukurani kwa kuuishi umama wao hata katika hali ngumu na changamoto za kiroho, zinazotokana na watoto wao kuamua kufuata wito wa kikuhani.

Kardinali Piacenza akihojiwa juu ya barua hii anasema, ni matokeo ya msukumo wa ndani ya moyo wake, katika kutafakari maisha ya wa mama wote wa Makuhani, Mapadre na waseminaristi ,pamoja na wanawake wote, walioyatolea maisha yao wakfu na walei pia, walioitikia mwaliko na kushiriki kazi za kitume kwa ajili ya adhimisho la Mwaka wa Mapadre, kama zawadi ya kiroho ya umama wao , mbele ya changamoto za wale walioitwa katika Utume wa kikuhani.

Wale wote, waliokubali kuyatolea maisha yao yote kwa ajili ya , sala, mateso na mafadhaiko, kuwa pia sehemu ya furaha yao, kwa ajili ya imani na kwa ajili ya utakaso wa kazi za Mungu, na hivyo kushiriki kwa namna ya kipekee , umama Mtakatifu wa Kanisa , kwa lina namna yake na utimilifu wake katika umama wa kimungu wa Maria.

Kwa ajli hiyo, Kardinali anaeleza, kutokana na habari kwamba Kristo anafanya kazi katika maisha ya wateule wake na wote walioitwa kuwa karibu zaidi nae , hakika inakuwa ni ushiriki wa kipekee, unaogusa pia maisha ya Mama wa Padre. Ni ya kipekee na maalumu kwa mama hao, hasa kutokana na ukweli wa faraja za kiroho,zinazotokana na furaha ya kwamba, ndani ya tumbo lake mmetoka kuhani wa Kristu. Kila mama wa Padre, katika ukweli wake hawezi kujizuia kufurahia kuona maisha ya mwanae halisi, si tu yamekamilika lakini yamevalishwa kwa nanma ya kipekee, upendo mtakatifu unaomkumbatia na kumbadilisha kwa ajili ya maisha ya milele.

Kardinali alieleza hilo huku akitaja kwa mfano, maisha ya Mtaktifu Monica kwa Mwanae Mtakatifu Augosotino , kama alivyoeleza Baba Mtakatifu Benedikito XVI, wakati akiyatafakari maisha ya Mtakatifu Augostino kwamba, husaidia Kanisa lote kufurahia, kwa mara nyingine tena, mchango mkubwa uliotolewa na Askofu wa Hippo kw aKanisa la Kristu, na pia kwa maendeleo ya ustaarabu wa binadamu.

Mtakatifu Monica, mama wa Augostino, hakika ni kielelezo cha wazi cha furaha ya Mama wote wazazi wa Makuhani. Sala, maombi na machozi ya Mtakatifu a Monica, yaligeuka kuwa kicheko baada ya mwanae kuongokea Ukristo. Uchungu na wasiwasi wa Monica , ulipata baraka za Bwana wa neema ya uogofu , kwa ajili ya mwanae Augustino.
All the contents on this site are copyrighted ©.