2013-01-08 15:54:11

Nawe nenda ukafanye hivyo! Ujumbe wa Siku ya Wagonjwa Duniani kwa Mwaka 2013


Ujumbe wa Baba Mtakatifu Benedikto XV1, kwa ajili ya adhimisho la Ishirini na Moja la Siku ya Wagonjwa Dunianiumetolewa. Adhimisho hilo la kila mwaka tarehe 11 Februari huenda sambamba kumbukumbu ya kiliturujia Mama Yetu Bikira Maria wa Lourdes, inayoheshimiwa sana kama kimbilio la wagonjwa. .

Ujumbe wa Papa unaitaja Siku ya Dunia kwa ajili ya Wagonjwa, kuwa siku ya kuwakumbuka wagonjwa, wafanyakazi na wahudumu wa afya, na kwa ajili ya waamini na watu wote, kwa ukarimu wao , fadhila , sala, kushirikishana na kugawana sadaka ya mateso ya wagonjwa, kwa ajili ya mema ya Kanisa. Na pia ni siku inayotoa wito kwa watu wote, kutambua uso huu wa mateso kwa ndugu zetu wake kwa waume,wanaokabiliwa na mateso ya maradhi, kupitia kwao kuuona Uso Mtakatifu wa mateso ya Kristu, ,aliye teswa , kufa na kufufuka kwa ajili ya kuleta wokovu wa watu " (Taz. Waraka wa Yohane Paulo II, kwa ajili ya Siku ya Dunia ya wagonjwa 13 Mei 1992 , 3).

Katika mazingira hayo, Baba Mtakatifu Benedikto XV1, ametaja hisia zake, kwa namna ya kipekee, kiroho , atakuwa karibu na wapendwa wagonjwa wote, wawe wanapata huduma za tiba hospitalini au majumbani , na wote wanaoishi katika hali ngumu za majaribu kwa sababu ya udhaifu wa maradhi na mateso. Kwao wote Papa anawafariji na maneno yaliyoandikwa katika Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, "Hamja achwa wapeke au kwamba hamna maana, lakini mmeitwa na Kristu , kuwa kioo cha Sura yake Teswa. .

Ujumbe wa Papa pia unawasindikiza wote wanaofanya hija za Kiroho katika madhabau ya Lourdes, eneo linalo julikana kuwa ishara ya matumaini na neema, akiwataka wafanye hija yao, kwa kuutafakari mfano wa Msamaria Mwema (taz. Lk 10 :25-37), katika kuelewa upendo wa kina wa Mungu kwa ajili ya kila binadamu, hasa wale wanaoteseka na ugonjwa au maumivu.

Papa ameeleza na kurejea maneno yaliyo hitimisha mfano wa Msamaria Mwema, "Nenda ukafanye vivyo hivyo" (Lk 10:37), akisema, Bwana anamtaka kila mwanafunzi wake , kufanya hivyo kwa ajili ya wengine, hasa wale wahitaji. Amesema, kama waamini, tunahitaji kuteka toka upendo huu usio na kipimo wa Mungu, kwa njia ya kujenga uhusiano thabiti pamoja naye, kupitia maombi na kuziishi hali za mashaka na wasiwasi, kwa ajili ya watu wengine , katika maisha yetu ya kila siku. kama ilivyo katika mfano wa Msamaria Mwema. Kwa wale wanao teseka kimwili na kiroho pia, watu wenye kuhitaji msaada wetu. Kuwajali na kujua hali ya mapungufu na mateso yao.

Papa anaasa hili si tu kwa wahudumu wa kichungaji au huduma ya afya, lakini kwa kila mtu, hata kwa ajili ya wagonjwa wenyewe, ambao uzoefu wao katika hali ya ugonjwa na mtazamo wa imani: inaweza kuwa faraja na msaada kwa wengine, kuikubali hali kwua mgonjwa, na kwa njia hiyo kutafuta maana ya maisha na njia ya kujenga muungano thabiti na Kristo, na kuuona upendo wa Kristu usio na kipimo "(SPE Salvi, 37).

Papa pia amerejea tafakari za mafundisho ya Mbalimbali wa Kanisa, wakiiona sura ya Yesu kwa msamaria mwema; na katika mtu aliyevamiwa na wezi, na ubinadamu uliojeruhiwa na kuharibiwa na dhambi yake, kama homilia za Watakatifu Origene, Ambrogio na Augostine.

Na pia katika mwaka huu wa Imani, ambamo tunapaswa kupanua wema na fadhila katika jumuiya zetu, ili kwamba kila mmoja wetu anaweza kuwa msamaria mwema kwa wengine, na hasa kwa wale walio karibu nasi. Kwa ajili ya hili Papa amewakumbuka wote ambao idadi yao haiwezi kuhesabika katika historia ya Kanisa waliosaidia wagonjwa kufahamu thamani ya binadamu na ya kiroho ya mateso yao, ili wapate kumtumikia kama mfano na kutia moyo, kama Mtakatifu Teresa wa Mtoto na Yesu wa Uso Mtakatifu(Novo Millenio Ineunte, 42), .

Papa amemalizia ujumbe wake kwa kutambua na kutoa himizo kwa taasisi zote za Katoliki zinazotoa huduma za afya na pia vyama na taasisi za kiraia, majimboni na katika jumuiya za kikristo, kwa familia na mashirika ya kidini, na wote wanao jishughulisha na huduma ya kichungaji katika uwanja huu wa afya , na watu wa kujitolea, Ili wote watambue kikamilifu, kwamba, "leo hii Kanisa , licha ya kuishi katika hali mbalimbali, msingi wa utume wake, unabaki kuw ani uelule wa kuufikisha upendo na ukarimu wa kweli wa Kristu, kwa kila binadamu, hasa wale ambao ni dhaifu na wagonjwa.

Papa amekabidhi adhimisho hili la Ishirini na moja la Siku ya Dunia ya Wagonjwa katika maombezi ya Mama yetu wa neema, anayeheshimwa sana katika madhabahu ya Altötting, na apate daima kuongozana wale ambao wanaokabiliwa na kutafuta faraja na tumaini thabiti, ili wapate kuuona uzuri kuwa Msamaria mwema , kupitia ndugu zao , wake na waume, wanao taabika kwa ugonjwa na mateso.All the contents on this site are copyrighted ©.