2013-01-08 15:22:10

Amani haitangamani na haki za binadamu - Papa


Jumatatu Baba Mtakatifu Bendikto XV1, akitakiana Heri za mwaka mpya na Mabalozi waliodhaminishwa katika Jimbo la Papa, toka Mataifa mbalimbali, alisema, Ujenzi wa amani daima huambatana na ulinzi na utetezi wa haki msingi za binadamu. Jukumu hili hata kama linafanikishwa katika njia nyingi mbalimbali na kwa viwango tofauti , inabaki kuwa changamoto kwa nchi zote, daima kuvuviwa na kuongozwa na hadhi ya utu wa Mtu na misingi ya kanuni zilizofumbatwa katika asili ya binadamu.
Papa alitaja, la kwanza muhimu kati ya yote, ni heshima kwa maisha ya binadamu katika hatua zake zote za tangu mimba kutungiwa hadi pale anapofariki katika hali za kawaida. Kwa mtazamo huo, Papa alionyesha kufurahia azimio la a Bunge la Mabunge ya Ulaya, lililopitishwa Januari mwaka jana,ambalo lilipiga marufuku euthanasia, kwa uelewa kama mauaji ya kukusudia na ni tendo la kutotimiza wajibu kwa binadamu tegemezi.. Wakati huohuo, Papa alionyesha kusikitika kwamba, katika nchi mbalimbali, hata zile zenye mapokeo ya kikristo, Juhudi zinafanyika kuanzisha au kupanua sheria za kuruhusu uchaguzi wa mimba na utoaji wa mimba. Utoaji wa mimba wa makusudi, unao lenga kusitisha au kufikisha mwisho wa mwanzo wa maisha katika njia yake asilia, ikiwa kinyume kabisa cha sheria ya maadili.
Papa ameeleza, Kanisa Katoliki kukataza hili, si kwamba halitambui au linapuuza, au hali na huruma na mateso yanayowakabili baadhi ya akina walio katika lika la uzazi. Kanisa linafahamu na kujali. Lakini pia linawajibika kuwa macho na sheria zinazotaka kudhulumu maisha ya wengine hasa ambayo bado ni teke yasiyo weza kujitetea wenyewe. Kanisa linatetea uwiano halali, kati ya haki ya maisha ya mama na mtoto ambaye hajazaliwa, haki kwa wote sawia mama na Mtoto. Papa alieleza huku akionyesha kujali, maamuzi ya hivi karibuni ya Mahakama Marekani ya Haki za Binadamu Kuhusu utungishaji mimba kiholela katika vyupa kwenye maabara, akisema huko ni kudhoofisha utetezi wa maisha yasiyozaliwa bado.

Papa pia alionyesha kusikitishwa, hasa na nchi za Magharibi, ambako kwa mara nyingi mtu anatiwa utata katika kupata maana ya haki za binadamu na wajibu wake, ambako kwa mara nyingi, haki inachanganywa na kujitukuza kwa mtu binafsi mwenye kujiona amejikamilisha mwenyewe binafsi , na kujionyesha hana tena nafasi ya kukutana na Mungu na watu wengine. Mtu aliyemwezwa na utafutaji wa maslahi yake binafsi kwa ajili ya kuiridhisha nafisi yake, k akutumia migongo hasa ya wasioweza kujitetea. Papa anasema, kwa watu hao, thamani na utetezi wa maisha ya watu wengine hauna tena maana. Lakini wanapaswa kukumbushwa kwamba, mtu hata kama anajiona kuwa amejikamilisha , bado anahitaji uwepo wa mwingine. Na hivyo, Papa ameasa, utetezi na ulinzi wa kweli wa haki za binadamu, ni lazima uzame katika fikira za mwingiliano wa binadamu , katika kipimo cha mtu binafsi na mitazamo ya kijamii.
All the contents on this site are copyrighted ©.