Umoja wa Afrika wapongeza uamuzi uliofikiwa kati ya Sudan ya Kusini na Sudan Kongwe
Dr. Nkosanza Dlamini Zuma, Kamishina wa Umoja wa Afrika amepongeza uamuzi wa pamoja
uliofikiwa kati Rais Omar Hassan Al Bashiri na Rais Salva Kiir Mayardit katika mkutano
wao uliofanyika mjini Addis Ababa, kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 5 Januari 2013, chini
ya usimamizi na uongozi wa Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini, Thabo Mbeki ambaye aliteuliwa
kuwa ni mpatanishi katika mgogoro wa pande hizi mbili.
Umoja wa Afrika unaendelea
kusisitizia umuhimu wa viongozi wa nchi hizi mbili kutekeleza kwa vitendo mambo msingi
yaliyofikiwa katika mkutano wao uliofanyika kunako tarehe 27 Septemba 2012 kuhusu
mipaka ya nchi hizi mbili. Lengo ni kuimarisha misingi ya haki, amani na maendeleo
endelevu, kwa kuwajengea wananchi wa Sudani ya Kusini na Sudan Kongwe ari na moyo
wa kujiamini katika mchakato wa kujiletea maendeleo endelevu; wakishirikiana kwa pamoja
ili kutafuta mafao ya wengi, katika nchi hizi na Bara la Afrika, katika ujumla wake.