2013-01-07 16:33:30

Hotuba ya Papa kwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao katika Jimbo la Papa


Baba Mtakatifu Benedikto XV1, Jumatatu amekutana na Mabalozi wanaowakilisha mataifa mbalimbali yenye kuwa na mahusiano ya kidiplomasia na Jimbo Takatifu, kama ulivyo utaratibu wa kila mwanzo wa mwaka, kutakiana heri na fanaka za mwaka mpya na Mabalozi hao.
Kwa muhtasari hotuba ya Papa kwa mabalozi, imezungumzia juu ya amani, kipeo cha uchumi na utetezi wa heshima ya maisha. Amesema ujenzi wa amani miongoni mwa jamii, si lelemama au hadithi ya kufikirika lakini amani inapaswa kuwa hali halisi za maisha ya watu kila siku. Na ameangalisha katika mwelekeo wa wimbi la umaskini kutaka kujitanua zaidi,akihimiza juhudi zaidi za pamoja kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo. Na amerudia kutoa wito wa amani kwa mataifa hasa yale yanayokabiliwa na vipeo vya ghasia na mapigano kama huko Syria, Congo , Nigeria n.k.
Jimbo la Papa lina uhusiano wa Kidiplomasia na mataifa 179, pamoja na vyombo vingine vya kimataifa kama umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, utawala wa kijeshi kama kisiwa cha Malta na mamlaka zingine kama Mamlaka ya utawala Palestina.
Papa ametaja bayana lengo kuu la Kanisa Katoliki, kuwa na mahusiano haya ya kidiplomasia ni kukuza amani na mshikamano wa binadamu duniani.
Papa aliianza hotuba yake na shukurani kwa hotuba nzuri iliyotolewa na Dekano wa Mabalozi, Balozi Alejandro Valladares Lanza na Makamu wake Balozi Jean Claude Michael, ambamo walimtaja Papa kuwa ana ujasiri wa kipekee katika kukabiliana na changamoto mbalimbali bila ya kukata tamaa.
Na kwa namna pekee, aliwasalimu Mabalozi wote wapya waliohudhuria mkutano huu kwa mara ya kwanza, akisema, uwepo wao ni ishara ya thamani na muhimu katika uhusiano na shuhuda za kazi za Kanisa Katoliki katika Mamlaka za kiraia ulimwengu. Na hasa katika kuonyesha njia ya mazungumzo na majadiliano, kuwa msingi na moyo wa mshikamano wa kina katika yote, mitazamo ya kiroho na kimwili, kwa ajili ya utendaji wa wema na fadhili kwa watu wote wake kwa waume, kila mmoja katika nafasi yake , na umuhimu wa kuendeleza Utu na hadhi ya binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.
Kwa roho hiyo, Papa aliongeza, Jimbo la Papa, hushiriki katika kazi za mikutano na mazungumzo mbalimbali ya Mashirika ya Kimataifa na Taasisi, si tu kwa sababu nyepesi za utoaji wa mchango wa wake wa kihali katika sekta kadhaa za kijamii, lakini hasa kwa ajili ya kufanikisha amani na utulivu miongoni mwa jamii, kama msingi wa maendeleo na ustawi wote wa binadamu.
Papa pia, ametaja ziara alizofanya mwaka uliopita kimataifa ambamo alitembelea Mexico, Cuba na Lebanon, na kupata nafasi ingine ya kuuthibitishia ulimwengu dhamiri za Kanisa kwa raia wa mataifa hayo kwamba, ni kukuza Utu wa binadamu na misingi ya amani.
Na pia alimkubuka kw anamna ya pekee , Marehemu Askofu Mkuu Ambrose Madtha, Mjumbe wa Jimbo la Papa nchini Ivory Coast, ambaye aliyefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari , pamoja na dereva wake.

Papa aliendelea kuizungumzia amani, iliyotangazwa na Mwinjilisti Luka, wakati wa mkesha wa Noel akisema, amani hayo si matunda ya kazi za binadamu lakini ni ushiriki halisi wa upendo wa Mungu kwa binadamu.
Na matokeo mabaya ya kumsahau Mungu , hayawezi kutenganishwa na matokeo ya ujinga wa kutouona uso wa Mungu katika ukweli, ujinga uliotiwa giza na mizizi ya ushabiki wa kidini usiokuwa na kipimo, kama kwa mara ingine ilivyojionyesha katika utendaji wa mashabiki hao katika kipindi cha mwaka 2012, ambamo baadhi ya raia wema walifanywa kuwa wahanga wa utendaji huo mbovu usiokuwa na kipimo.
Utendaji ulionyesha kwa mara ingine dini kutumiwa vibaya, na kupotoshwa kutoka lengo lake la kuwa chombo cha kuwapatanisha wanaume na wanawake na Mungu, na kama nuru na utakaso wa dhamiri, inaoonyesha wazi kwamba kila binadamu ameumbwa kwa Sura na mfano wa Muumba wake Mungu.

Papa alieleza kwa kuzitazama hali katika mataifa mbalimbali , kama ilivyokuwa huko Mashariki ya Kati –Iraki, Jerusalem, Palestina . Na pia alirejea katika ukanda wa Jangwa la Sahara, ambako amekuwa akihimza juhudi za kipekee kwa ajili ya ujenzi wa amani na hasa katika maeno yaliyojeruhiwa na vita, watu wakiitafuta haki na uhuru wa kweli hasa katika kuikiri imani yao. Na kwa namna ya pekee alikumbuka pembe ya Afrika, na Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako vitendo vya ghasia vimelazimisha watu kuzikimbia nyumba zao familia na mazingira yao, na kwenda kuishi uhamishoni .
Na pia amelitaja taifa la Nigeria, ambako mashambulizi ya kigaidi, yamevuna wahanga wengi waamini na hasa miongoni mwa watu waliokuwa wamekusanyika katika sala. Amabako maeneo ya Ibada, makanisa na mahekalu ya sala , yanashinikizwa kuwa maeneo ya hofu na mgawanyiko, badala ya kuwa mahali pa amani na utulivu. Kwa namna ya pekee Papa alisikitishwa na taarifa za kuuawa kwa baadhi ya Wakristu wakati wa adhimisho la Siku Kuu ya Noel. Aidha Papa ameonyesha kujali uharibifu uliofanyika huko Mali, ghasia zilizo haribu hata alama zenye thamani kubwa kimtaifa. Pia kinacho endelea katika Jamhuri ya Afrika Kati .

Papa anasema katika hali hizo zote , anapenda kukumbusha kwamba, Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican uliotolewa miaka hamsini iliyopita, chini ya usimamizi wa Mtumishi wa Mungu, Papa Paulo VI, Ujumbe uliopelekwa na Kanisa la Ulimwengu kwa viongozi wote wa dunia , unabaki kuwa muhimu. Kwa namna ya Pekee unahimiza moyo wa kuwa wajenzi wa amani miongoni mwa watu wote . Na kwamwe isisahaulike kwamba, Ni Mungu pekee, mfanikishaji wa taratibu za amani duniani. Kwa maeneo hayo, Papa aliwatakia Mabalozi wote na wasaidizi wao na familia zao Matashi mema ya mwaka mpya wa 2013 , na kuwashukuru wote, Asanteni Sana.All the contents on this site are copyrighted ©.