2013-01-02 09:54:54

Jubilee ya miaka 150 ya kifo cha Mtumishi wa Mungu Pauline Jaricot na miaka 50 ya utambuzi wa fadhila za kishujaa


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Kardinali Paul Poupard, Rais mstaafu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni kuwa mwakilishi wake katika Sherehe za kuhitimisha Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 150 tangu alipofariki dunia Mtumishi wa Mungu Pauline Jaricot na miaka 50 tangu Kanisa lilipotambua fadhila za kishujaa; maadhimisho ambayo yatafanyika hapo tarehe 9 Januari 2013, mjini Lione, nchini Ufaransa.

Kardinali Paul Poupard ataongozana na Monsinyo Francois Duthel, Msimamizi mkuu wa mchakato wa kumtangaza Mtumishi wa Mungu Pauline Jaricot kuwa Mwenyeheri pamoja na Mheshimiwa Padre Daniel Carnot, ambaye aliwahi kuwa ni Mkuu wa Shirika la Kimissionari Barani Afrika.All the contents on this site are copyrighted ©.