2013-01-01 11:20:31

Sala ya Kanisa kwa ajili ya kuombea Amani Duniani kwa mwaka 2013


Liturujia ya Neno la Mungu katika maadhimisho ya Siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu ilihitimishwa kwa Sala ya Waamini kwa kuomwombea Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita pamoja na Maaskofu ili katika kutekeleza shughuli zao za kichungaji wajikite katika kutafuta haki, majadilinao na amani miongoni mwa watu wa mataifa.

Bikira Maria Mama wa Mungu awasaidie Viongozi wa Serikali, watunga sheria na wanasayansi kuheshimu umama ambao ni zawadi kubwa ambayo binadamu amekabidhiwa na Mwenyezi Mungu.

Bikira Mtakatifu Mama wa Mkombozi pamoja na Mtakatifu Yosefu, waliomlinda Mtoto Yesu kwa upendo thabiti, awasaidie wazazi na walezi kuwa kweli ni walimu na mashahidi wa imani kwa watoto wao.

Bikira Maria Mama wa Mungu awaombee na kuwajalia zawadi ya amani mataifa yote yanayoteseka kutokana na vita, ili uhuru na utu wa mwanadamu viweze kuheshimiwa na kuthaminiwa na wote. Awasaidie waamini kushuhudia furaha ya kua ni wafuasi wa Kristo kwa kutangaza na kushiriki katika ujenzi wa Ufalme wa Mungu.

Sala ya waamini imetolewa katika lugha ya Kireno, Kiarabu, Kiswahili, Kifaransa na Kipolandi. Kwa upande wa lugha ya Kiswahili, sala imesomwa na Sr.Esther Malamso kutoka Shirika la Masista wa Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asilia la Ivrea.

All the contents on this site are copyrighted ©.