2012-12-29 14:11:44

Viongozi 12 wa Kanisa waliuwawa katika kipindi cha Mwaka 2012


Mama Kanisa anaufunga Mwaka 2012 kwa kuwakumbuka watoto wake kumi na wawili waliofariki dunia, wakiwa katika harakati za kumtangaza Kristo kama sehemu ya utume na maisha yao. Kuna Mapadre kumi waliouwawa, mtawa na mlei mmoja. Kwa takribani miaka minne kwa sasa Amerika inaongoza kwa mauaji ya Mapadre duniani, kati ya Mapadre kumi waliouwawa, sita wanatoka Barani Amerika.

Bara la Afrika linafuatia kwa kumwaga damu ya Watangazaji wa Habari Njema ya Wokovu. Mapadre watatu na mtawa mmoja waliuwawa Barani Afrika. Kuna Padre na Mtawa mmoja waliouwawa Barani Asia. Maisha ya Watangazaji Injili yaliyomiminwa kwa ukatili yanaendelea kuwa ni mbegu ya kukomaa kwa Ukristo sehemu mbali mbali ya dunia.







All the contents on this site are copyrighted ©.