2012-12-27 15:26:23

Mwaka wa Imani - Padre Andrej Koprowski


Mkurugenzi wa Mipango ya Utangazaji Redio Vatican, Padre Andrea Koprowski, akitafakari mwaka wa Imani, katika muktadha wa mwaka mpya 2013 anasema, dunia inaendelea kushuhudia hali ngumu na wengi kukosa uhakika wa namna za kujinasua na hali hiyo.
Padre Koprowski, anataja ,sababu msingi inayoleta hali hiyo, kama kama alivyotaja pia Mwenye Heri Yohane Paulo II, kuwa ni "miundo ya dhambi", yenye kushinikiza kwa nguvu kubwa, jamii kutengana, shinikizo lenye kutaka kuharibu yote. Lakini kwa upande mwingine kuna dalili za mshikamano mpya, unaolenga kuimarisha mazuri kwa watu wote. Umoja unaolenga kuwa msaada katika ujenzi wa maisha yaliyostaarabika kwa siku za baadaye, yenye kupelekaji mbele hisia nzuri , miongoni mwa jamii na moyo wa umoja, katika maana ya maisha ya furaha.
Kwa muono mwepesi wa raia wa kawaida , kuna utambuzi wa hitaji la kufanya mabadiliko katika mambo muhimu , mtu akianza na yeye mwenyewe. Mabadiliko katika mtindo wa maisha na matarajio ya malengo ya mafanikio katika vigezo vya kuthamini, hatima ya matendo mema katika maisha ya kila, kwa Mkristu.
Padre Koprowski ameeleza na kurejea Katekesi ya Papa Benedikto XV1 ya Desemba iliyopita, ambamo alitaja kwamba, wito wa utendaji katika misingi ya Imani ya Kikristu, hauzuiwi na mipaka ya kibinadamu, kuishiriki historia ya wokovu na ukweli kwamba, binadamu ameumbwa na Mungu. Na kwamba kila mmoja ameteuliwa na Mungu, hata kabla ya kuumbwa ulimwengu.
Na kupitia Mwana Wake Yesu Kristo, uteuzi huo na upendo wake unajionyesha hadi hatima yake Msalabani na katika ufufuko wake. Uteuzi huo , unahusiana na mwelekeo katika hatima yake, iliyojaa roho ya upendo. Nasi kama wafuasi wake, kwa njia ya neema ya Yesu Kristo, ambamo tumepata wokovu na mshamaha wa dhambi , tumetakaswa na kukombolewa kwa damu yake. (Efe 1:10).

Hivyo Mkristu anaitwa kufungua mitazamo yake, kwa ajili ya utu wa mtu na kwa ajili ya amani ya kijamii katika dunia ya leo , ambamo mna vizingiti vingi dhidi ya amani.
Na Papa Benedikto XV1, katika homilia yake kwa ajili ya Ibada ya Misa Takatifu Krismasi mwaka huu amehoji: "Je, tuna muda na nafasi kwa ajili ya Mungu, licha ya ufanisi wa kazi unaofanikishwa na teknolojia mpya yenye kuokoa muda? Na ni nini maana ya kuwa na Mungu? Papa ameonya, hitaji la kujiweka karibu na Mungu inaonekana si muhimu tena. Muda wetu wote unaonekana tayari kumejaa. mambo ya kidunia. Mungu hapewi nafasi. Hili ni jambo la hatari .

Padre Koprowski anakumbusha kwamba, maisha ya mtu kujiweka karibu na Mungu huangazia unyeti na azma ya kurejesha utu sahihi kwa mtu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na kukombolewa kwa damu ya Yesu. Ni maisha yanayotazama maisha ya kila siku katika familia, sehemu za kazi, na pia jamii na utamaduni wake kwa ujumla. Ni msisitizo wa maisha ya Kiinjili, kiini cha njia maisha na wito wa Ukristo.

Padre Koprowski anaendelea kusema, licha ya matatizo mbalimbali ya kisaikolojia na kijamii - upendo ni nyenzo yenye nguvu katika kuwaunganisha na kuwanyunyua pamoja: upendo na huruma, hurejesha hadhi ya kila mmoja. Na mgogoro wa sasa, unatokana na kukossekana kwa nyenzo hii muhimu katika jamii. Mwelekeo wa watu kutothamini tena njia ya Kiinjili , imesabab isha uharibifu mkubwa katika maadili muhimu ya binadamu. Ni uharibifu mkubwa katika maisha yote ya kistaarabu. Imani kwa maisha ya pamoja imepungua na watu kumezwa na ubinafsi na chuki.
Padre Koprowski,ametaja utendaji wote wa Kanisa Katoliki katika maisha ya Kijamii, lengo lake kuu ni kumboresha kila binadamu kiroho na kimwili , ni udumishaji wa hadhi na utu wa mtu, aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.








All the contents on this site are copyrighted ©.