2012-12-26 08:58:43

Wasomi jengeni uhusiano mwema na Yesu Kristo muweze kufahamu maana na hatimaye, kufurahia maisha!


Yesu Kristo ndiye Mkombozi pekee wa binadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti. Anahitaji kukutana na wasomi ili kuwaonesha maana halisi ya maisha na furaha ya kweli inayobubujika kutokana kwake. RealAudioMP3

Hii ni changamoto kwa wasomi kujitahidi kumjifunza na kumwelewa Yesu Kristo na hatimaye, kujenga uhusiano wa dhati pamoja naye kwa njia ya: maisha ya Sala, Tafakari ya Neno la Mungu, Sakramenti za Kanisa pamoja na Matendo ya huruma.

Hii ni sehemu ya ujumbe wa Noeli kwa Mwaka 2012 kutoka kwa Mheshimiwa Padre Charles Kitima, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania, SAUT kwa wasomi na wanazuoni sehemu mbali mbali za dunia. Anawaalika wasomi hao kumjifunza Yesu Kristo kisayansi, kwa kutoa nafasi katika maisha na vipaumbele vyao, hapo watakuwa na fursa kubwa ya kufahamu maana ya maisha, utu, heshima na hatima ya binadamu kwa siku za usoni.

Padre Charles Kitima katika mahojiano maalum na Radio Vatican anawaambia wasomi na wanazuoni kwamba, wakibobema katika haya, kwa hakika watakuwa na furaha ya kweli katika maisha yao! Mengine yote yanapita, lakini Kristo ni yule yule, Jana, Leo na Hata Milele, Yeye ni Omega, Mwanzo na Mwisho; nyakati zote ni zake.







All the contents on this site are copyrighted ©.