2012-12-26 15:28:35

Mkesha wa Noel, sita wafariki kwa shambulio Kanisani- Nigeria


Kipeo cha mashambulizi dhidi ya Wakristu Nigeria bado ni kitisho. Jumanne wakati wa adhimisho la Siku Kuu ya Noel, maghaidi wenye silaha walishambulia Kanisa katika Jimbo la Yobe, Kaskazini mwa Nigeria. Shambulio lililosababisha watu sita kufariki duniani kati yao akiwemo Padre. Na pia nyumba zisizopungua 20 kuchomwa moto na watu wanaodhaniwa kuwa mashabiki wa Kiilslamu, wa kikundi cha Boko Haram.
Kikundi hicho kikiwa na silaha kali, kilishambulia kanisa wakati Wakristu wakiwa katika Ibada ya Mkesha wa Noel katika eneo la vijijini la Peri, nje kidogo ya Mji wa Biashara wa Potiskum. Washambuliaji hao. Hili ni shambulio jingine la umwagaji wa damu ya watu wasiokuwa na hatia,
Akito maelezo juu ya mashambulio hayo , Rais wa Chombo kinacho waunganisha Wakristu Nigeria (CAN), Mchungaji Ayo Oritsejafor, kw amasikitiko makubwa ameyaita mashambulio hayo, kuwa ni kitendo cha kinyama dhdi ya watu wanaotumia haki yao ya kuabudu kwa amani.Na kwamba, huo ni uchoikozi na M maudhi yasiyo kifani, na unyama mkubwa. Na ni kuwa kinyume kabisa na imani ya dini yoyote ile ianyosadiki kwa Mungu.
Amewasihi wananchi wema wa Nigeria, kutoanzisha mashabulizi dhidi ya uchokozi huo, na badala yake , waendelee kukemea vikali uhalifu huu na kuchukua hatua madhubuti si kwa njia ya jicho kwa jicho lakini , kupitia njia ya majadiliano na elimu ya umma kama hatua za kukomesha unyama huo. Na wasiyakimbia maeneo yao ya kuzaliwi, bali wabaki katika makazi yao, kwani ipo siku amani na utulivu vitarejea.
Baba Mtakatifu Benedikto XV1, Jumanne wakati akitoa ujumbe wake kwa jiji na dunia, alilikumbuka taifa la Nigeria na kukemea mashabulio ya kighaidi yanayoendelea kumwaga damu za watu wasiokuwa na hatia katika taifa hilo.
Papa ameomba kuzaliwa kwa Kristu na kuwezeshe kurudisha amani na mapatano nchini Nigeria, ambako matendo ya ugaidi mkatili unaendelea kuvuna waathirika, hasa miongoni mwa Wakristo.
Na pia Mkombozi wa dunia na awe msaada na faraja kwa wakimbizi kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kwa ajili ya amani nchini Kenya, ambako pia kumekuwa na mashambulizi ya kikatili kwa raia wema, na maeneo ya kuabudu.








All the contents on this site are copyrighted ©.