2012-12-25 16:18:28

Toeni muda wenu kwa wahitaji na Mungu, Papa amehimiza.


Baba Mtakatifu Benedikto XV1,Jumatatu Usiku aliongoza Kanisa la Ulimwengu, kusherehekea Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana wa Noel , kwa kuongoza ibada ya Mkesha wa Noel katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Ibada iliyohudhuriwa na maelfu ya waamini na kutangazwa katika vyombo vya mawasiliano duniani kote.
Papa akitoa mahubiri katika Ibada hiyo, alitoa swali kwa waamini na wasioamini, iwapo wanapata nafasi katika maisha yao nyenye hekaheka na shughuli nyingi, maisha yanayoendeshwa na teknolojia, nafasi kwa ajili ya watoto na maskini na Mungu? RealAudioMP3







All the contents on this site are copyrighted ©.