2012-12-25 12:29:21

Mzee Nelson Mandela atembelewa Hospitalini ili kutakiwa matashi mema ya Siku kuu ya Noeli


Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini, katika maadhimisho ya Siku kuu ya Noeli kwa Mwaka 2012, amemtembelea Mzee Nelson Mandela wenye umri wa miaka tisini na nne, ili kumtakia kheri na baraka kwa Siku kuu ya Noeli, wakati huu anapoendelea na matibabu, akiwa amelazwa Hospitalini.

Rais Zuma anasema, Mzee Madiba anaendelea vyema na matibabu na ameonesha furaha ya kutembelewa na wageni wakati huu wa Noeli na kwamba, Madktari na wauguzi wake wanaridishwa na mwenendo mzima wa afya yake kwa sasa.







All the contents on this site are copyrighted ©.