2012-12-24 16:02:53

Penye ukarimu safi na nyenyekevu, Mungu yupo - Papa


Elizabeth kutembelea na Maria si ishara tu ya fadhila lakini pia unyenyekevu.



Ni mahubiri ya Baba Mtakatifu Benedikto XV, Jumapili mchana , baada ya sala ya Malaika wa Bwana, kwa mahujaji na watalii na wageni waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Hotuba ya Papa iliangalisha tena katika somo la Injili la Jumapili ya nne ya Majilio, ambamo Bikira Maria anamtembelea binamu yake, Elisabeth.

Tukio hili, alieleza Papa, si tu linawasilisha kitedo cha fadhila , lakini pia huonyesha kwa njia nyepesi, kukutana kwa Agano la Kale na Agano jipya. Na pia huonyesha jinsi Neno la Mungu lilivyokuwa na nguvu kwa binadamu,kama tunavyo soma Elizabeth licha ya umri wake mkubwa uliokuwa umebadilisha maubile yake na kuwa tasa, kwa nguvu ya neno la Mungu alipata Mimba, na kuwa na saburi ya kuzaa mtoto. Papa ameitaja tukio hili kuwa ni ashirio kwa Israel, kumsubiri Masiya waliye mtegemea kuja.

Papa pia alizifaafanua hisia za Elisabeth, kwa salaam yake kwa Maria, "Heri wewe, umebarikiwa katika wanawake wote,zikionyesha kutumia kwa maandiko, yaliyotolewa, katika Maandiko Kiebrania, kwa wanawake shupavu wa vita , ambao juhudi zao ziliokoa taifa la Israel hatarini. RealAudioMP3












All the contents on this site are copyrighted ©.