2012-12-20 14:46:31

Dhamana ya Kanisa kwa ajili ya amani Afrika


Katika Sinodi Pili ya Maaskofu maalum kwa ajili ya Afrika, iliyofanyika Oktoba 2009, majadiliano yalilenga jinsi Kanisa Katoliki barani Afrika, linavyo weza kusaidia kuweka misingi ya maridhiano kwa jamii yenye haki zaidi na amani. Maamuzi ya Sinodi hiyo pamoja na maamuzi ya Sinodi ya Pili iliyofuatia iliyotoa waraka wa Africae Munus, vinaonyesha mwelekeo wa utendaji na mwaliko kwa Kanisa zima, kuchukua msimamo wazi na daima kuwa, "Chumvi ya dunia."

Pamoja na kwamba, katika siku za nyuma, watu wa Kanisa walionyesha kupenda kushiriki katika utafutaji wa majawabu ya matatizo na migogoro inayopambanisha jamii , walifanya hivyo mara nyingi, kama mtu binafsi. Kwa kweli, mapema katika miaka ya '90, wakati jamii za Afrika inapita katika kipindi cha mpito, kutoka mfumo wa chama kimoja cha kisiasa, na kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya kisiasa, katika kipindi hicho, Maaskofu waliambatana na jamii, kufanya marekebisho, toka mfumo wa chama kimoja hadi vyama vingi.
Maaskofu waliitikia vyema, maombi yaliyotolewa na Mikutano ya usimamizi huru ya kitaifa, ambamo waliombwa kutoa fafanuzi zaidi juu ya ufunguo mpya wa demokrasia, na umuhimu wa wananachi wenyewe kushiriki katika hatua za kimaendeleo kidemokrasia, kama sheria mpya ya ushindani wa kisiasa, kwa ajili ya ufanikishaji haki na amani.
Tunakumbuka, jinsi viongozi wa Kanisa walivyotoa mchango wao katika hili, kwa kutaja wachache Mons. Isidore De Souza wa Benin, Mons Ernest Kombo Kongo, Mons Philippe Kpodzro katika Togo, na Mons. Laurent Monsengwo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Akitoa Azimio la mwisho la Sinodi ya Pili ya Maaskofu Maalum kwa ajili ya Afrika , Azimio la “Africaè Munus”( Dhamana ya Kanisa Afrika), Baba Mtakatifu Benedikto XV1, ametoa mwaliko wa kuiga mfano wa viongozi hao.
Papa amehimiza jumuiya zima ya Kanisa kuwa chombo madhubuti cha kufanikisha maridhiano, haki na amani, barani Afrika, kwa kutambua uhai wa Kanisa. Papa amelipa Kanisa Afrika, jukumu katika maisha ya kijamii, kuwa mjenzi wa Afrika moja yenye mapatano, na yenye kutawaliwa na amani na upendo. Kwa ajili ya kupambana na changamoto hii, imependekezwa kwa Makanisa, kuanzisha mipango ya utekelezaji imara na kuunda taasisi zenye uwezo wa kujenga majiundo mpya kidhamiri.
Hati ya Africae Munus si tu inapendekeza walei kuiishi imani yao kwa njia ya matendo ya kisiasa, lakini pia inahimiza wachungaji kuwa wadhamini wa amani na maridhiano barani Afrika, ambako milipuko ya migogoro na ukiukaji wa hadhi ya binadamu wa kusitisha, unazidi kuongezeka katika baadhi ya nchi, na hasa ambako Waislamu huzuia Wakristo kuiishi imani ya dini yao kwa amani.

Tunawezaje kuacha kuwafikiria , katika wakati huu wa maandalizi kwa ajili ya Siku kuu ya Noel, Wakristo Nigeria, Kenya na Somalia, walivyojawa wasiwasi na hofu ya nini kinaweza kutokea, wakati Kanisa lina sherehekea, kuzaliwa kwa Mfalme wa Amani?
Ni muhimu kwamba kanisa linakuza mazungumzo kati ya dini, na mazoezi kiroho ,yenye kuhimiza waamini kujifunza kufanya kazi kwa pamoja na mashirika ya kikazi, kukuza amani na haki, uaminifu na kuheshimiana.
Kwa mtazamo huo, Hati ya Africae Munus, inawaalika walei Katoliki kuhimiza majadiliano na ushirikiano na wafuasi wa dini nyingine, na hivyo kuwa mashahidi wa imani na maisha ya Kikristo.

Kama ilivyotokea siku za nyuma, wakati viongozi wa Afrika walitoa maombi yao, kwa watu wa Kanisa, wasaidia kufanikisha watu wa Afrika wajinasue na migogoro ya kisiasa. , ambayo hadi leo hii watu wa Afrika wanatambua utendaji wa kanisa kama ni ishara ya matumaini. Tumaini si tu linaloweza kuwaongoza katika kupata suluhu kwenye mizozo, lakini pia katika mwelekeo wa jamii kuwa na utaratibu wa haki.

Kwa kweli, mwaka mmoja baaada ya kuchapishwa kwa Hati ya Dhamana ya Afrika, Maaskofu wa Afrika, wanaweza kuwa na mwelekeo mzuri, pamoja na uwepo wa mipaka , katika utendaji kwenye mwelekeo huu: kwa mfano, Kanisa la Nigeria, kupitia mashauriano thabiti, bado linawatia moyo Wakristu wadumishe imani yao na wasivunjwe moyo na utendaji wa Waislamu wasiovumilia wengine, badala yake wakatae kuingia kwenye mduara wa vurugu.

Maaskofu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hivi karibuni walikutana na wanachama wa chama cha Movement M23, Septemba 19, 2012 na kuw ana Ibada ya Misa maalum katika parokia ya Mtakatifu Alois wa Rutshuru (eneo lililo chukuliwa na kikundi cha waasi), na walikemea, vita madhulumu na vitendo vingine haramu, wakiomba udumishaji wa umoja kwa watu wa Kongo.

Baada ya mgawanyiko wa Sudan na kuwa nchi mbili huru, Maaskofu wametoa jibu la umoja na udugu, kwa kudumisha Baraza moja la Maaskofu kwa mataifa hayo mawili. Hiyo imekuwa ni ishara ya mshikamano kwa Wakristo wa Sudan zote mbili, kuw Kanisa ni moja na maisha yake ni ya kidugu maisha. "

Kama ilivyopendekezwa na Africae Munus, Kanisa Afrika, ni kanisa linalo sikia umuhimu wa daima kuwepo mahali ambapo maamuzi thabiti hufanyika kwa ajili ya mustakabali wa watu wa Afrika. Na hivyo , tutumaini kwamba, utakuwepo uwakilishi wa kuonekana, kutoka Kongomano la Maaskofu wa Afrika na Madagascar, katika muktadha wa Umoja wa Afrika na mashirika mengine ya kikanda na kitaifa ya utekelezaji.
Maaskofu pia wanatumaini utendaji wake utaweza kutoa matunda ya kutosha , na kuwa mshiriki wa nguvu, na kwa mapana zaidi, katika mikutano inayoandaliwa barani , au mahali pengine, kwa ajili ya upatikanaji wa majawabu yanayofaa zaidi kutatua migogoroya Afrika.

Changamoto kubwa, ni Kanisa Afrika, kuwa na utendaji utakao weza kutoa matunda kwa wingi, na kuwa mshiriki mkuu katika njia mpya za mawasiliano jamii , ili sauti yake isikike zaidi licha ya kuwa na utendaji dhahiri.

Imeandikwa na Marie José Muando Buabualo, Idhaa ya Kifaransa kwa ajili ya Afrika.








All the contents on this site are copyrighted ©.