2012-12-19 14:50:29

Twitter: Ukitaka kutembea katika mwanga, jitahidi kuongozwa na Neno la Mungu; furaha ya kweli inapatikana kwa kuungana na Mungu!


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita mara baada ya Katekesi Jumatano tarehe 19 Desemba 2012, ametuma ujumbe wake kwa njia ya mtandao wa kijamii wa twitter akisema kwamba, hija ya imani ina nyakati kuu mbili: mwanga na giza. Kama mwamini anapenda kutembea daima katika mwanga, basi haja budi kuongozwa na Neno la Mungu.

Sehemu ya pili ya twitter ya Baba Mtakatifu inasema kwamba, Bikira Maria aliweza kufurahia ujumbe kwamba, atakuwa ni Mama wa Yesu, Neno wa Mungu aliyefanyika mwili. Anasema, furaha ya kweli inajikita katika kuungana na Mwenyezi Mungu.

Hii ni twitter na sita kutumwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, tangu alipozindua matumizi ya mtandao huu wa kijamii, ambao hadi sasa una zaidi ya wafuasi millioni mbili na sabini elfu. Wafuasi katika akaunti ya Baba Mtakatifu @ Pontifex kwa lugha ya Kiingereza wamekwisha vuka millioni moja na laki mbili; kwa lugha ya Kihispania kuna wafuasi 465,000 na katika lugha ya Kitaalia kuna wafuasi 200,000.







All the contents on this site are copyrighted ©.