2012-12-19 07:41:59

Mapadre mtakuwa maskini sana ikiwa kama mtaanza kujiahangaikia, kujitafuta na kutopea katika ubinafsi!


Katika Maadhimisho ya Mwaka wa Imani, tunaendelea kuambatana na Askofu mkuu Yuda Thadeus Ruwaichi wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania anayetupatia tafakari ya kina kuhusu unabii na madai yake na Makasisi wanapaswa kuwa ni Askari wa Kristo, tayari kutekeleza utume wao bila ya kujibakiza wala kumezwa na malimwengu. RealAudioMP3

Leo katika makala haya, anaendelea kupembua maana ya kukesha katika maisha ya Familia ya Mungu, yaani kuwa tayari daima kutekeleza mapenzi ya Mungu, kushughulikia na kuchuchumilia maisha ya uzima wa milele. Ni mwaliko wa kutumia vyema elimu, karama na vipaji mbali mbali ambavyo wamekirimiwa kwa ajili ya Mungu na Kanisa lake. Popote pale Padre anapotumwa lazima ajitahidi kujenga nyumba yake ambayo ni Kanisa, kwa kulipenda, kulitokea jasho, kulitumikia na kulihangaikia kwani ndivyo inavyotakiwa na Kristo mwenyewe.

Askofu mkuu Ruwaichi anawakumbusha Mapadre kwamba, watakuwa maskini sana pale watakapojitafuta na kujihangaikia wenyewe na hatimaye kutopea katika ubinafsi badala ya kujitosa kimasomacho kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake. Kristo aliyeteswa, akafa na kufufuka awe ni mfano hai katika maisha na majitoleo ya Mapadre. Kamwe wasiogope kugharimika na kupata hasara kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake katika malimwengu!







All the contents on this site are copyrighted ©.