Tahariri ya Padre Federico Lombardi kwa wiki hii, imetazamishwa katika Ujumbe wa Papa
kwa ajili ya siku ya Amani Duniani, 1 Januari 2013. Ujumbe wenye jina "Heri wapatanishi,"
kama ilivyoandikwa katika Injili. Wale ambao kwa imani kwa Mungu na ahadi zake "mara
nyingi hubezwa au kupuuzwa na walimwengu. Lakini Papa anasema, watu hao huweza kuuonja
uzoefu wa maisha ya furaha kama zawadi toka kwa Mungu. Padre Lombardi, ana ainisha
kwamba, Ujumbe wa Papa unakwenda kinyume na mitazamo mingi ya kileo. Unatoa msisitizo
kwamba, "sharti la amani" ni "kuvunja udikteta wa itikadi na dhania za kutoamini
Mungu, zenye kuzuia utambuzi wa sheria asili ya maadili, iliyoandikwa na Mungu katika
dhamiri ya kila mtu." Hivyo ujumbe, anarudia kuangalisha juu ya utetezi wa maisha
, ndoa na juu ya uhuru na haki katika daku za utambuzi. Na si tu katika mazingira
ya mgogoro wa kipeo cha sasa, mnamo sisitizwa kazi za kijamii kitaifa, haki ya kufanya
kazi ,lakini katika ukweli wake, tatizo la njaa ni baya zaidi kuliko hata kipeo cha
fedha , na juu ya umuhimu wa kuwa na mfumo wa maendeleo, usiotanguliza juu faida
na maslahi binafsi lakini utendaji kwa ajili manufaa ya wote, na kuthamini zawadi
asilia zinazopatikana bure. Kwa amani, tunaweza kuelimika na kuwa na muono wa
mbele zaidi juu ya familia, shule na jumuiya za kidini na kiraia, pamoja na ufundishaji
wa kweli na umakini katika utoaji wa maneno, ishara na mitazamo. Miaka hamsini
iliyopita, Papa Yohane XXIII, ilitoa waraka wake maarufu "Amani Duniani ,(Pacem
in Terris)" akisema, “ nguzo ya amani ni ukweli, uhuru, upendo na haki”. Amani ni
utaratibu usio tangamana na upendo. Hivyo inakuwa ni kufikiria mahitaji ya wengine
na kufanya sehemu na mali zao , kuwa sehemu yetu pia. Pengine yote haya yanaonekana
kama ndoto , lakini sisi wote tunajua kwamba ni haki. Hebu tujaribu tena, amemalizia
Padre Lombardi.