Kardinali Filoni akutana na Waseminaristi wa Jimbola Arua.
Kardinali Leonardo Filoni , Ijumaa akiwa Uganda pia alipata nafasi ya kuwatembelea
Seminaristi wa Arua. Katika hotuba yake , alilenga katika swali jepesi , nini lengo
la kuwa seminarini au kwa maneno mengine ya kueleweka zaidi nini maana ya majiundo
haya katika mwelekeo wa kuwa kuhani. Alitoa ufafanuzi kwa maswali hayo, akiangalisha
katika Injili ya Mtakatifu Marko, juu ya kuzaliwa kwa jumuiya ya kitume, kama ilivyoandikwa
katika sura ya tatu , ambamo Yesu aliteua kumi na wawili ... Yesu anaunda jumuiya
mpya , kitendo cha ubunifu na kuwaunda ili waweze kuwa pamoja nae na ili aweze kuwatuma
kwenda kuhubiri Injili . Katika muktadha huu wa imani, basi, ni muhimu kuwa na
taarifa na uelewa, kuwa na akili wazi na kujifunza, kukumbuka daima utu wa Yesu Kristo,
asili ya ukweli na kweli. Na alihitimisha hotuba yake kwa kuwashirikisha furaha
za utakatifu katika kuwa wanafunzi wa Yesu, wenye kuwa na hamu ya kutambua wito
wake. Awali ya yote,alisema, ni kukuza na kuwa na upendo mkubwa kwa Yesu Kristo katika
Sakramenti hii ya Ukuhani. Heri wao wanaoingia katika utumishi wa Sakramenti hii!
Yeye sasa ni kweli katika Ekaristi, hivyo ni kujitahidi kujifunza na kumjua vizuri
zaidi na kubaki katika umoja naye, na kutenda kila jambo kwa Imani kubwa kwake.
Pili, daima kuwa waaminifu kwa Kanisa na Mafundisho yake – na daima kuufanya upendo
wake ujulikane , kuwa tayari kubeba ushahidi wake, hata katika majitoleo ya sadaka
ya utakatifu wa kuifia dini, mbele ya watu . Hatimaye, mwe watu jasiri na imara wa
Mungu, katika hali zote, kwa sababu maisha ya kikristo ni jambo zuri! (Taz. Flp 4.,
4). Kardinali alikamilisha hotuba yake kwa kutoa swali kwa wote, kama mseminaristi
ataka ukuhani wa aina gani? Je ni kuhani anaye mshuhudia Kristo kwa sababu anaamini,
anampenda, na ndiye anayemwonyesha hatua za utendaji katika maisha? Ni aina gani ya
kuhani anataka kuwa kwa ajili ya Kanisa, baada ya nusu karne ya Mtaguzo Mkuu wa Pili
wa Vatican. Je ni tayari kuchukua urithi alioupata kwa kujengwa kwa njia ya kazi ngumu
na umwagaji wa damu, isiyokuwa na hatia ya mashahidi wengi, wamisionari watakatifu,
na wake kwa waume wa Imani? Je, Kristo na Kanisa ni matumaini yake? Ni kujiuliza,
Je, mimi kweli miko tayari kuwatumikia katika daraja hili la ukuhani kwa usafi
wa moyo, kama zawadi ya jumla ya Kristo? Je, nina moyo wa Kristo kujenga kanisa
na kufanya uinjilishaji katika karne ya Ishirini na moja. Jibu unalo wewe, alisema
Kardinali Filoni .