2012-12-13 08:44:36

Rev. Dr. Jovitus Mwijage ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa PMS Tanzania


Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu amemteua Mheshimiwa Padre Jovitus Mwijage kutoka Jimbo Katoliki Bukoba kuwa Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa ya Kazi za Kimissionari nchini Tanzania kwa kipindi kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2017.

Uteuzi huu umeanza kutekelezwa hapo tarehe 23 Novemba 2012. Mheshimiwa Padre Mwijage alizaliwa kunako tarehe 2 Desemba 1966. Alipadrishwa takribani miaka kumi na saba iliyopita. Baada ya kufanya utume mbali mbali kama Paroko usu, mhasibu na mlezi wa Seminari Ndogo ya Rubya Bukoba, alipelekwa mjini Roma kuendelea na masomo na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu kuhusiana na Historia ya Kanisa kutoka katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian.







All the contents on this site are copyrighted ©.