2012-12-12 09:15:55

Watumiaji wa mitandao ya kijamii! Kumekucha mjini Vatican!


Ndugu msikilizaji wa Radio Vatican, zifuatazo ni anuani kwa lugha mbali mbali ambazo zinakuwezesha wewe kutwitter na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kwa njia ya mitandao ya kijamii. Huu ni mtandao ambao unazinduliwa rasmi tarehe 12 Desemba 2012, katika Kumbu kumbu ya Bikira Maria wa Guadalupe.

Itakumbukwa kwamba, tukio hili liliwasilishwa kwa waandishi wa habari mjini Vatican hapo tarehe 3 Desemba 2012. Waliobahatika kuwasiliana na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita katika akaunti yake binafsi @pontifex watajibiwa ili kuzima kiu yao kuhusu imani.

Kihispania @pontifex_es
Kiitaliani @pontifex_it
Kireno @pontifex_pt
Kijerumani @pontifex_de
Kipolandi @pontifex_pl
Kiarabu @pontifex_ar
Kifaransa @pontifex_fr

Habari kutoka Vatican zinabainisha kwamba, mtandao huu wa kijamii utaendelea kuongeza lugha mbali mbali kadiri inavyowezekana. Bila shaka, iko siku moja hata watumiaji wa mitandao ya kijamii wataweza kuwasiliana na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita kwa kutumia lugha ya Kiswahili, lakini kwa sasa, tuvute subira kwani mambo mazuri wanasema Waswahili hayahitaji haraka!







All the contents on this site are copyrighted ©.