2012-12-12 14:37:33

Papa aanza kutwitter na watumiaji wa mtandao wa twitter! Mambo makuu haya!


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, mara baada ya katekesi yake, Jumatano tarehe 12 Desemba 2012 amezindua rasmi matumizi ya mtandao wa kijamii unaojulikana kama Twitter, kwa kuonesha furaha yake ya dhati kwa kujiunga na mamillioni ya watumiaji wa mtandao huu. Amewapatia baraka yake kama sehemu ya kwanza ya ujumbe wake.

Baba Mtakatifu amesaidiwa na maofisa kutoka Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Jamii pamoja na wanafunzi wawili kutoka Chuo Kikuu cha Villanova wanaofanya kazi katika Baraza la Kipapa.

Twitter ya kwanza kutoka kwa Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ni utangulizi, baadaye, Baba Mtakatifu mwenyewe, ataanza kujibu baadhi ya maswali yaliyochaguliwa kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Baadhi ya majibu yametolewa muda mfupi tu baada ya Baba Mtakatifu kuzindua matumizi ya mtandao wa twitter. Kwa sasa watumiaji wa mtandao wa twittwer wanaweza kutwitter na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, kuhusu masuala ya Imani.







All the contents on this site are copyrighted ©.