2012-12-11 15:45:04

Ujumbe wa Noel wa WCC: Mwanga wa Kristu, Nuru ya kuongoza hatua zetu.


Ujumbe kwa ajili ya adhimisho la Noel kwa mwaka huu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa la Dunia (WCC) unaongozwa na Maneno : “Mwanga wa Kristo, ni nuru inayo angazia hatua zetu na kutuonyesha njia ya haki na amani".

Ujumbe huo, wa Katibu Mkuu wa WCC, Mchungaji Olav Fyske , wenye kuwa na maneno ya matumaini, umetumwa kwa jumuiya za waamini zaidi ya 300, ambazo ni sehemu ya mwili wa kiekumeni.

Gazeti la Italia , L’ Osservatore Romano, limenukuu sehemu ya ujumbe huo , uliochota aya za Biblia, wenye kusisitiza dhamira ya Wakristo, katika kukabiliana na unyanyasaji na dhuluma zinazo athiri ulimwengu wa Kileo. Imebainishwa kwamba, Maneno ya , aya hizo zitaongoza Mkutano Mkuu wa Kumi wa WCC , Utakao fanyika kutoka Oktoba 30 - Novemba 8, 2013 Busan, Korea ya Kusini.
Ujumbe huo umevuviwa na aya kutoka katika kitabu cha Isaya "Je, Mwanzi uliopondeka hatauvunja wala utambi utokao Mosi hatauzima , atatokeza hukumu kwa ukweli, Isaya "(42, 3), na Injili ya Yohane:" Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda "(1, 4-5).
Mandhari ya amani na haki katika hali ya watu leo hii, itakuwa ni kati ya kazi za Mkutano Mkuu wa 2013, unaotajwa kuwa nafasi kwa ajili ya tafakari za pamoja. Hivyo itakuwa ni kutakafari hali halisi za tangu mada hiyo kutolewa mwaka 2001, muogo mmoja uliopita , kutazama utendaji wa WCC, katika hoja za kidharura za kujitolea na ujenzi wa uelewa juu ya majanga ya ubaguzi na unyanyasaji. "Muongo uliolenga kutokomeza Ukatili" kama lililo jina la mpango ulioanzishwa na WCC mwaka 2001 na kumalizika mwaka 2011.

Mchungaji Fyske anasema, "Tunajua katika kipindi hiki cha muongo mmoja, kulikuwa na mawazo mengi yalitolewa katika majadiliano na utendaji halisi, wengi walijishughulisha na ukomeshaji wa unyanyasaji, katika ueelwa kwamba, ni dhalilisho na dhambi, lakini pia tunajua pia kwamba bado kuna mengi ya kufanyika”.








All the contents on this site are copyrighted ©.