Amerika Kusini, Caribbean, Marekani na Canada ni nyumbani kwa ukatoliki, kwa kuwa
nusu ya idadi ya Wakatoliki duniani iko katika eneo hilo. Hilo lilielezwa Jumatatu
wakati wa kufunguliwa kwa Mkutano wa Kimataifa wa Marekani zote mbili unaofanyika
kwa ajili ya maadhimisho ya kutimia kwa miaka 15 tangu kutolewa kwa hati ya Kichungaji
na Mwenye Heri Yohane Paulo 11 , baada ya Sinodi ya Maaskofu iliyofanyika kwa ajili
ya Kanisa barani Amerika ya Kusini na Amerika ya Kaskazini, Caribbea na Canada, mwaka
1999.
Baba Mtakatifu Benedikto XV1, akitoa hotuba wakati wa Ibada ya Misa,
iliyoongozwa na Kardinali Marc Ouellet, Mkuu wa Decania ya Maaskofu Katoliki, aligusia
"ukarimu i" na "roho wa umisionari, ulivyokuwa tangu mwanzo wa Kanisa katika eneo
hilo. Mkutano huu unahudhuriwa na washiriki 250 kutoka eneo hilo linalojulikana kama
Mabara mapya.
Kardinali Marc Ouellet, katika homilia yake wakati wa Ibada,
alilitaka “Bara mpya ' kudumisha roho wa kiinjili na umisionari ulioonekana tangu
Ukristu kuingia katika eneo hilo , na liwe mstari wa mbele katika Uinjilishaji Mpya.
Lijibidishe katika kuimarisha juhudi za kufikisha Imani Katoliki katika maeneo ambayo
bado kuguswa, Kaskaini na Kusini, kupitia juhudi za kuimarisha ushirikiano na uratibu
kati ya makanisa mahalia na kujenga ustaarabu wa upendo.
Kuwe na juhudi za
kulitambulisha na kuliinua Kanisa kupitia ushauri na muono wake,katika kumaliza
migogoro na tofauti za kimbali itikadi, kidini na siasa, kupitia njia ya majadiliano
na kuheshimu utu wa mtu, na familia ya mke na mme, na katika kujali matatizo mengine
ya Kijamii. Alihimiza kipeo cha kijamii kinachoendelea sasa ni wakati muafaka wa kueneza
na kuzungumzia nguvu ya Kristo, ambayo ni upendo, kwa kuanzia ndani ya familia. Aidha
aligusia suala la wahamiaji na ghasia zinazo shamirishwa na mitandao ya biashara
ya madawa ya kulevya na matumizi yake ya ovyo kuongezeka. Lakini juu ya yote, Kardinali
ilionyesha kujali zaidi mashambulizi dhidi ya utamaduni wa maisha na taasisi ya ndoa
na familia, ambapo alielezea kama tatizo la bara zima, na haja ya kulinda uhuru wa
dini.
Na Dk Guzmán Carriquiry, Katibu Mkuu wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya
Amerika ya Kusini, kitengo cha mahusiano kati ya Makanisa katika mataifa ya mabara
haya, akishiriki Mkutano huu, alitaja migawanyiko inayojitokeza mara kwa mara. Na
alipongeza Sinodi 1997 kwamba, ilikuwa ni ni sehemu ya kuvunja tabia ya kutilia mashaka,
badala yake imefanikisha kuleta umoja zaidi kwa viongozi wa Kanisa Marekani.
Na
Mlei Carl A. Anderson , Mkuu wa Chama cha Knights of Columbus, kinacho dhamini kazi
za matendo ya huruma ya Papa katika mataifa ya Amerika ya Kusini, akizungumzia mabadiliko
ya kiroho, alisema, uponyaji huu unapaswa kuanzia tangu katika kuelewa maana ya sakramenti
ya ndoa ya Kikristu . Na haiwezekani kuendeleza utume wa Uinjilishaji Mpya , bila
kwanza kutangaza kwa bidii ukweli juu ya binadamu na utu wake . Kama Wakristu tunapaswa
kutangaza kwa ushupavu na ushawishi wa kweli juu ya ndoa na familia . Kwa maana hiyo
, Wakristu leo hii wanaitwa katika Uinjilishaji Mpya , ambamo wao wenyewe wanatakiwa
kwanza kuongoka na kuyaonyesha maisha Katoliki ya kweli.
"Kinachotakiwa ni
si tu mipango mipya ya kichungaji kwa wale ambao hawaukubatii tena Ukristu , ingawa
bado ni muhimu kufanya hivyo , pia tulenge zaidi kwa wale4 ambao habari hii njema
ya upendo bado kuwafikia. Uinjilishaji Mpya lazima upanuke zaidi na uwe na chanya
zaidi katika upeo". Aliendelea "ni kutoa ujumbe unaoongea nguvu ya Kristo, ambayo
ni upendo ... kwa kuanza ndani ya familia na kuchanua hadi kwa jamii nzima kwa ujumla.
Na
alionyesha kujali haja ya kidharura, juu ya watu masikini na wale wanaoteseka kwa
sababu mbalimbali msingi zilizo nje ya uwezo wao. Alikumbusha nchi za Magharibi,
kuwa ni maeneo yenye rutuba ya upendo na fadhila, mnamo weza kustawi tena moyo wa
ubinadamu wa kuajaliana , kama ilivyokuwa karne za nyuma. Ni tu kwa kujenga ustaarabu
wa upendo Wakatoliki wanaweza kuwa na mshikamano wa kweli na umoja wa kikanisa Marekani
".
Alikamilisha kwa kuangalisha katika Ujumbe wa Mama yetu ya Guadalupe na
katika maisha ya St Juan Diego, i unaoonyesha dhahiri wito wenye lishe mpya ya utangazaji
wa Injili kwa Kanisa zima, na kwa kila mtu na taifa.