2012-12-10 15:25:12

Jumuiya ya Taize yaomba malazi kwa ajili ya washiriki wa mkutano.


Jumuiya ya Kimataifa ya Vijana ya Taize, inatoa ombi kwa watu wote wenye mapenzi mema hapa Roma kufanikisha nafasi za malazi zaidi ya elfu kumi , kwa ajili ya vijana wageni, toka pande zote za Ulaya.

Madhumuni ya vijana hao kumiminika Roma, ni kushiriki katika Mkutano wao wa siku nne, unaoanza tarehe 28 Desemba hadi 2 January 2013 . Huo utakuwa ni Mkutano wao wa Kimataifa wa Kiekumene wa 35.

Jumuiya ya Kimataifa ya Taize inatoa ombi la malazi kwa wote wenye nafasi majumbani mwao , hapa Roma na vitongoji vyake, iwe ndani ya familia, jumuiya za kidini, watu binafisi , wazee, vijana taasisi na mashirika pia. Na imeliita kuwa ni ombi la kidharura , kwa kuwa zimebaki siku kumi tu kuwasili kwa vijana hao toka Hispania, Urusi, Uswiss, Croatia na mataifa mengine ya Ulaya.

Kwa mujibuw idadi iliyojiandikisha ni vijana 35 elfu wanaotazamiwa kuwasili kwa ajili ya tukio hili, linalotajwa pia kuwa sehemu ya hija katika mwaka huu wa imani , hija inayongozwa na Mada Mbiu ; Kujenga ulaya ya mshikamano , utandawazi na kazi za Kijamii katika kuwapokea wageni: mbinu za kupambana na ghasia , dhidi ya umaskini na ubaguzi.
Hija hii ya vijana katika jiji la Roma, inawahusu vijana wenye umri kati ya miaka 17-35. Wanakusanyika si kwa sababu za kinadharia lakini wanataka kupata uzoefu wa kweli , katika kuishi pamoja katika maisha ya sala na kugawana kinacho patikana.
Vijana, licha ya kugawanyika katika vikundi vikundi kulingana na walikotoka,bado wanapania kimaisha, kuivunja mipaka ya k ijiografia na ubinafsi si kwa ajili ya kutafuta kile kinacho watengenisha lakini kujenga umoja na mshikamano katika yale yanayowaunganisha.
Si kwa sababu za msorajua lakini kuyaachia maisha katika ishara za matumaini. Wanakuja kwa ajili ya kugundua mizizi ya jumuiya moja ya watu, waliozama katika kuzitazama kwa makini , hali halisi za masiha yasiyo kuwa na mipaka au ubaguzi wa kisiasa au kimakundi au kivyama.
Kwa wenye nafasi ya kulaza wageni wanaweza kupiga simu namba o6,77,266.266, au kutumia Email: info,roma@taize.it, 389,83,533,00, stampa.roma@taize.it








All the contents on this site are copyrighted ©.