Papa anaomboleza kifo cha Patriaki Ignazio wa IV Hazim
Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, ametuma salam za rambi rambi kwa Askofu
mkuu Spyridon wa Jimbo kuu la Eliopoli, kufuatia kifo cha Patriaki Ignazio IV Hazim,
wa Kanisa la Kigiriki la Kiothodox kwa Mashariki yote, kilichotokea hivi karibuni.
Baba Mtakatifu anaungana na wote wanaoomboleza msiba huu kwa kuondokewa na
mchungaji wao mkuu kwa njia ya sala. Marehemu Patriaki Ignazio IV Hazim, enzi ya uhai
wake, alijitoa katika kutangaza Injili, akaonesha ushuhuda wa mwanga angavu wa imani
na mapendo; akawahimiza Wakristo wake kuchuchumilia upatanisho, haki na amani miongoni
mwa Jumuiya ya Kimataifa. Ni kiongozi aliyechuchumilia kwa dhati kabisa majadiliano
ya kiekumene kati ya Makanisa haya mawili, ili wote waweze kuwa wamoja chini ya Kristo.
Mwishoni,
Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, anapenda kuwahakikishia waamini wote wanaoteseka
kutokana na sababu mbali mbali uwepo wake wa karibu pamoja na kuendelea kuombea amani
huko Mashariki ya Kati.