2012-12-07 08:52:25

Rais Joachim Gauck wa Ujerumani akutana na Papa Benedikto XVI mjini Vatican


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Alhamisi tarehe 6 Desemba 2012 amekutana na kufanya mazungumzo na Bwana Joachim Gauck, Rais wa Shirikisho la Ujerumani na baadaye kiongozi huyo na ujumbe wake, walikutana na Kardinali Tarcisio Bertone, katibu mkuu wa Vatican pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Vatican.

Viongozi hawa wamejadili pamoja na mambo mengine uhusiano mzuri kati ya Vatican na Ujerumani. Wamegusia mtazamo wa Kikristo kuhusu mwanadamu na changamoto zinazoendelea kujitokeza katika ulimwengu wa utandawazi. Wamebadilishana pia mawazo kuhusu masuala mbali mbali ya kimataifa: athari za myumbo wa uchumi kimataifa Barani Ulaya na mchango ambao Kanisa Katoliki linaweza kuchangia katika hali kama hii.







All the contents on this site are copyrighted ©.