Askofu mkuu Zimowksi kumwakilisha Papa kwenye Maadhimisho ya 21 ya Wagonjwa Duniani
kwa Mwaka 2013
Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amemteua Askofu mkuu Zygmunt Zimowski, Rais
wa Baraza la Kipapa la huduma za kichungaji kwa ajili ya wafanyakazi wa sekta ya afya,
kuwa mwakilishi wake maalum katika Maadhimisho ya Siku ya Ishirini na moja ya Wagonjwa
Duniani, itakayoadhimishwa hapo tarehe 11 Februari 2013, mjini Altotting, nchini Ujerumani.
Wakati
huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa
Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu kuwa mwakilishi wake kwenye Jubilee ya Miaka
50 ya Madhabau ya Bikira Maria wa Afya Njema, yaliyoko nchini India sanjari na maadhimisho
ya Jubilee ya Miaka 25 tangu Baraza la Maaskofu Katoliki India lilipoanzishwa. Sherehe
hizi zinatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 9 hadi 11 Februari 2013.