2012-12-06 16:19:30

Unajisi mpya: wajenga mshikamano zaidi kwa Wakristo


Wakristu wa Senegal wanasema uchokozi unaofanywa dhidi yao, unawafanikisha kujenga mshikamano na umoja zaidi kati yao na kwa imani yao. Hilo limetamkwa kufuatia uchokozi wa Jumapili ambamo watu wasiojulikana mapema sana asubuhi ya Jumapili iliyopita, waliinajisi sanamu ya Bikira Maria akiwa na Mtoto Yesu katika mikono yake, kw akuipondaponda kwa mawe.

Sanamu hiyo ilikuwa imewekwa katika mlango wa kanisa Katoliki, wilayani Assainies nje kidogo ya jiji la Dakar. Kitendo hicho kimeitwa ni uchokozi usio na kipimo, kwa watu waliostaraabika.

Kwa mujibu wa magazeti mahalia "Le Soleil" na "L'Observateur" , yaliyonukuliwa na Apic, kufuru hiyo ilifanyika Jumapili saa 11 za asubuhi. Habari hizi zimepokelewa kwa masikitiko na uchungu mkubwa na waamini na watu wastaarabu.

Rais wa Senegal Sall Macky, akiwa amesiktishwa na taarifa hiyo amesema, ni lazima waharifu watafutwe na kuwajibishwa kwa haki kisheria, kama hatua za kudumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya dini" katika taifa la Senegal lisilo egemea upande wowote wa kidini.

Hii ni mara ya pili kwa Wakristu kuchokozwa katika kipindi cha wiki chake kupita. Hapo tarehe 6 Oktoba, makaburi zaidi ya 160 ya Wakristu yaliharibiwa na watu wasiojulikana, katika eneo la makaburi ya Mtakatifu Lazaro wa Bethania na huko Bel Air ya mji mkuu wa Senegal.








All the contents on this site are copyrighted ©.